Mkuu wa kamati ya Matukio kutoka The Runners Club, Geofrey Mwangungulu  aliyeshika (kipaza sauti) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua mbio za usiku zitakazofanyika Agosti,29,2020.
 Rais wa The Runners Club, Utole Lema akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mbio za usiku zitakazofanyika Agosti 2,2020 kuanzia Ufukwe wa Coco, Magomeni hadi Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Globu ya jamii
THE runners wakishirikiana na Windhoek wazindua msimu wa Tatu wa mbio zinazofanyika (Dar night runner) zitakazofanyika Agosti 2, mwaka huu kuanzia Coco beach hadi Magomeni jijini Dar es Salam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa kamati ya Matukio kutoka The Runners Club, Geofrey Mwangungulu amesema kuwa mbio za mwaka huu zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Kilomita tano na Kilomita 15.

"Tutakuwa na mbio makundi mawili tutakuwa na mbio kilomita tano na mbio kilomita 15, kwahiyo tuko hapa kukuhamasisha wewe mwanamazoezi au mwanariadha kushiriki mbio hizo kuja kuimarisha afya na kung'aa katika tukio hili la kihistoria." Amesema Mwangungulu

Amesema kuwa mbio hizo zitafanyika kuanzia saa tano usiku (5:30 usiku) kuanzia Coco beach twalipo hadi  Magomeni kwa Kilomita saba na nusu kwenda na kurudi na kutimiza kilomita 15.

"Kuna njia mbalimali ambazo zimewekwa kwaajili ya washiriki na kuwa sehemu ya historia na kwenda kuweka historia Agosti 29, 2020, kuanzia saa tano na nusu usiku tutakuwa tukianza rasmi mbio zetu za mazoezi maeneo ya Coco beach Twalipo." Amesema Mwangungulu

Hata hivyo amesema kuwa kwa yeyote anayetaka kushiriki mbio hizo za usiku atajiandikisha kwa shilingi 40,000 kwenye aina zote za mbio hizo za usiku za kilomita tano na kilomita 15.

"Namna ya kushiriki na namna ya kujiandikisha taarifa zitawajia hivi karibuni." Amesema Mwangungulu

Hata hivyo amesema kuwa mshindi mwaka huu atapewa medali kwa wote walioshiriki mbio hizo na baada ya kumaliza shughuli ya mbio kutakuwa na burudani ya kihistoria katika ufukwe wa Coco beach kwa wote ambao watakuwa wamefanikiwa kwenda na kurudi katika fukwe za Coco

Kwa upande wake Meneja wa Rasilimali watu na utawala kutoka Windhoek, Simon Salatiel amesema kuwa wanaendelea katika kusaidia jamii kwa kudhamini mbio za Dar night ambazo hufanyika usiku.

"Mwaka jana tulifanya vizuri na tuliona ni uzoefu bora na watu walifurahi kwani watu wanatumia vinywaji na kunapokucha watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida."Amesema Salatiel.

Hata hivyo amewakaribisha wakazi wa jijini la Dar es Salaam, mikoa ya jirani kuja kushiriki mbio hizo kwani zinaboresha afya.

Amesema kuwa mbio za mwaka huu wameboresha zaidi katika burudani kwani kutakuwa na maDJ wazuri, ambao wataleta burudani hata kwa watu ambao hawataweza kukimbia.

"Karibuni sana mjipatie bia bora pamoja na mazoezi ili kupata uzoefu wa kupata kinywaji na mazoezi karibuni sana mpate fursa ya kushiriki, kuboresha afya zao pamoja na kuleta umoja katika jamii." Amesema Salatiel.

Mbio za usiku hii ni mara ya tatumfurulizo kufanyika jijini Dar es Salaam na mafanikio makubwa yanazidi kuonekana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...