MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imetumia gari maalum lililochorwa vibonzo kutolea elimu kwa Wananchi mbalimbali waliotembelea kwenye mabanda ya maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi, Simiyu.

Umati mkubwa wa watu umekuwa ukivutika kwa wingi katika banda la TMDA ambalo limekaa sambamba na gari hilo.

Afisa Habari na Elimu kwa Umma, James Ndege alieleza kuwa, TMDA mara kwa mara inahakikisha inabuni mbinu mbalimbali za kuhamasisha jamii juu ya wajibu wao katika kulinda afya zao.

Aidha, alisema katika kuwafikia wadau waliopo maeneo mbalimbali, Mamlaka imetoa ujumbe wa kukumbusha jamii juu ya wajibu wao kwa njia ya vibonzo ili kufikia jamii pana zaidi na kwa haraka.

Uhamasishaji huo wa vibonzo kupitia gari hilo maalum unahamasisha utoaji taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa ambayo imeonekana ni njia rahisi zaidi.

TMDA imekuwa ikitoa elimu kwa Wananchi juu ya ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaatiba na vitendanishi katika maonesho hayo ya Nanenane ambapo msimu huu ni mwaka wa tatu mfululizo yakifanyika Kitaifa kwenye viwanja hivyo vya Nyakabindi, Simiyu.
Afisa Habari na Elimu kwa Umma wa TMDA Bw. James Ndege akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea gari lenye ujumbe maalum kwa michoro ya vibonzo la Mamlaka hiyo katika maonesho ya Nanenane Nyakabindi, Simiyu mapema leo Agosti 8.2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...