Na Jusline Marco, Arusha

Viongozi wa makundi ya waendesha bodaboda wilaya ya Arusha,wamachinga na umoja wa madereva jiji la Arusha kwa pamoja wameahidi kushirikana na kundi la kijani la magufuli 2020 .

Wakizungumza katika Uzinduzi wa kundi hilo baadhi ya vijana kutoka katika chama cha mapinduzi CCM Mkoaji hapa wamesema kuwa lengo la kundi hilo ni kuhakikisha mgombea urais kupitia chama hicho kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu anapata ushindi.

Akizungumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa kundi hilo Victor Kolumba Moshi amesema kuwa kundi hilo limekusudia kumuunga mkono Mhe.Magufuli katika mchakato wa uchaguzi utakapoanza hasa wakati wa kampeini.

Aidha amesema kuwa umoja huo ambao upo nchi nzima makao yake  makuu yapo jijini Arusha ambayo kazi yao itakuwa ni kuyasajili makundi yanayoamini na kukubali kazi ambayo imefanyika kwa kipindi cha miaka mitano chini ya Dkt.John Magufuli.

Ameongeza kuwa pamojs na uundwaji wa kundi hilo pia baadhi ya makundi ambayo yameamua kuunga mkono juhudi hizo yameweza kusaini mkataba wa hiyari wa kutafuta kura za Dkt.John Magufuli 2020 muda na wakati utakapowadia.

"Hapa tunachokifanya siyo kampeni bali ni kuwasajili wajumbe wapya ambao wataenda kutafuta kura hizo,kwa hiyo isitafsiriwe na wale ambao wanapinga kila kitu wakidhani tumeanza kampeni mapema"Alisisitiza mwenyekiti wa chama hicho.

Naye mlezi wa chama hicho Fredrick John Mumbuli amesema kuwa yale mema yaliyofanywa katika awamu ya tano ndiyo yanayowafanya kuamua na kutia nadhiri kwamba wataungana na chama cha mapinduzi kumpigia kura Mhe.Magufuli pasipo kujali itikadi ya vyama vyao.

Kwa upande wake mdau wa maendeleo katika mkoa wa Arusha Moses Mashalla amesema kuwa kama wadau kazi yao ni kuhakikisha wanatangaza sera za rais kwa kuzunguka nchi nzima kuwaambia watanzania namna alivyosaidia kuboresha huduma ya elimu bila malipo,kuboresha mradi wa bwawa la umeme la bonde la rufiji.

"Tumeona kiasi cha shilingi bilioni 19 zimetolewa na serikali kufanya ukarabati wa shule zote kongwe nchini na katika sekta ya afya tumeona maboresho mengi."Alisema mdau huuo wa maendeleo

Bi.Amina Njoja ambaye ni mwenyekiti wa wamachinga katika jiji la Arusha amewaomba wamachinga wenzake kujutokeza katika uchaguzi mkuu kumpigia kura mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi kwanj ndiye mtu wa kwanza kiona chngamoto za wamachinga na kuwapatia vitambulisho ambavyo vimekuwa mkombozi kwao.

Vilevile ameomba umoja huo uzidi kuimarika na kuweza kutimiza lengo lililokusudiwa kwa kuungana na kuujenga Mkoa wa Arusha na kuleta maendeleo katika jamii.

Sambamba na hayo katibu wa kundi hilo Profit Mmanga amesema kuwa wamewakutanisha viongozi hao ili kuweza kuungana nao katika kumtafutia mgombea wao kura mwaka huu 2020 ma kueleza kuwa kampeni zitakapoanza makundi hayo waliokutana nayo kupitia viongozi wao watafanya kampeni ya nyumba hadi nyumba ili kuhakikisha kura hizo wanazipata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...