Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

WAKATI jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau zikiendelea kuhakikisha dawa ya viuadudu inatumika ipasavyo ili kutokomeza malaria nchini, baadhi ya wananchi wameonekana kutokuijua dawa hiyo na kuelezea njia wanazotumia kupambana na mbu waenezao malaria.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa  Wilaya za Ilala na Kigamboni jijini Dar es Salaam wameeleza kutokuijua dawa hiyo inayotumika kuua viluilui vya mbu huku wengine wakidai walishawahi kuisikia kwenye vyombo vya habari.

Wamesema kwamba endapo Serikali itatia mkazo na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu manufaa ya dawa hiyo na jinsi ya kuitumia wataweza kuondokana na kero ya kuumwa malaria mara kwa mara.

Kwa mujibu wa wananchi wa Wilaya hizo wametoa ombi kwa viongozi wa ngazi mbalinbali walioko kwenye wilaya zao kuhakikisha dawa hiyo ambayo inatengenezwa kwenye kiwanda cha kutengeneza dawa ya viuadudu kilichopo mkoani Pwani ikatumika kuua mbu katika mazalia yao na hiyo itaounguza watu kuugua maralia.

Hata hivyo awali alipotembelea kiwanda cha viuadudu kilichopo kibaha mkoani pwani Rais John Magufuli aliziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinanunua dawa hiyo na kushangazwa na kitendo cha nchi nyingine kunufaika na dawa hiyo lakini hapa Tanzania bado matumizi yake yanasuasua.

Meneja uzalishaji wa Kiwanda pekee Afrika cha kutengeneza viuadudu kilichopo Kibaha mkoani Pwani Gaspa Kimbi( kushoto)akimuonyesha Juma Amir mkazi wa Kigamboni jijini Dar es  Salaam  viluilui ambavyo ni mazalia ya mbu ambavyo vimekutwa katika eneo lake huku wakazi hao wakidai kutokuijua dawa ya viuadudu ambayo inaangamiza mazalia ya mbu.
Gaspa Kambi ambaye ni Meneja Uzalishaji katika Kiwanda cha kutengeneza Viuadudu akiangalia maji kama yana viuluilui vya mbu

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...