JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
C:\Users\RPC Office\Desktop\LOGO POLICE.jpg

JESHI  LA  POLISI  MKOA  WA  MWANZA  LINAWASHIKILIA  WATU  4  KWA  TUHUMA  ZA  MAKOSA    YA KUPANGA TUKIO  LA  MAUAJI  YA  MTU  MMOJA WILAYANI  UKEREWE.

TAREHE 25.08.2020 MAJIRA YA 02:00HRS USIKU ENEO LA MISSION, KATA YA NYAMANGA, KISIWA CHA UKARA, WILAYA YA UKEREWE, MKOA WA MWANZA, ANDREW MAGAI, MIAKA 48, MKARA, MKRISTO, MKULIMA WA KIJIJI CHA CHIBASI, ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA KUKATWA NA VITU VINAVYODAIWA KUWA NA NCHA KALI KWA MADAI KUWA MAREHEMU KABLA YA KIFO CHAKE ALIWASAFIRISHA WATU AMBAO HAWAKUTAMBULIKA KWENDA KUVUNJA NYUMBA YA MAGESA SIMON @ WILE.

UCHUNGUZI WA AWALI UMEBAINI KUWA TUKIO LA KUVUNJA NYUMBANI KWA MAGESA SIMON @ WILE LILIKUA NI LA KUTENGENEZWA ILI KUHALALISHA MAUAJI YALIYOTOKEA ENEO HILO. UCHUNGUZI WA KINA UNAENDELEA UKIHUSISHA WATAALAMU MBALIMBALI. MWILI WA MAREHEMU ULIFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI KATIKA KITUO CHA AFYA BWISYA NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU KWA MAZISHI.




WALIOFIKISHWA MAHAKAMANI LEO 31/08/2020 NI:-

  1. MAGESA SIMON @ WILE, MIAKA 50, MKALA, MKULIMA, MKAZI WA NYAMANGA.
  2. MAKANJE MGETA, MIAKA 28, MKARA, MKAZI WA KIJIJI CHA CHIBASI.
  3. MKAPA MAGESA@SIMON, MIAKA 24, MKARA, MKULIMA, NYAMANGA.
  4. SELESTINI DATUSI, MIAKA 22, MKEREWE, MKRISTO, MKULIMA, NYAMANGA.

WATUHUMIWA WOTE WAMEFIKISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KUJIBU TUHUMA ZINAZOWAKABILI. 

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKA WANANCHI, WANASIASA WA VYAMA  VYOTE  KUTOJIINGIZA KATIKA MAMBO AMBAYO YANAWEZA KUHAMASISHA UVUNJAJI WA SHERIA NA KUVURUGA AMANI NA UTULIVU WA NCHI, LIMEAPA KUENDELEA KUCHUKUA HATUA KALI KWA KILA ATAKAYEKIUKA SHERIA.

IMETOLEWA NA:-
Muliro JUMANNE MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

31 AUGUST, 2020

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...