Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga B. Agnes Mtawa.



*********************************
Na. Catherine Sungura-WAMJW,Dodoma.
Wauguzi na Wakunga ambao watakuwa
hawajahuhisha leseni zao ndani ya miezi sita kuchukuliwa hatua, ikiwemo
kufutwa kwenye daftari la Uuguzi na Ukunga, hivyo kutoruhusiwa kutoa
huduma kwenye vituo vya afya vya umma au binafsi.
Hayo yamesemwa leo na Msajili wa
Baraza la Uuguzi na Ukunga Bi. Agnes Mtawa kwenye kikao kazi cha
kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi wauguzi wakuu wa
wilaya kinachoendelea jijini Dodoma.
“Nitoe rai kwa Wauguzi na Wakunga
ambao hawajahuisha leseni zao ndani ya miezi sita, sheria inamtaka
msajili awafute katika daftari la Uuguzi na Ukunga, na kama watafutwa
hawatakuwa na sifa ya uuguzi na ukunga”. Alisema Bi. Mtawa.
Aidha, Msajili huyo alisema hadi
sasa ni asilimia 75 ya wauguzi na wakunga wameshahuisha leseni zao na
asilimia 25 waliobaki bado wanaendelea kuangalia kwenda kanzidata yao
kwani wapo wauguzi ambao pengine wamefariki, kustaafu na wengine
wamebadilisha kada ila kwa wale ambao bado bado wanatoa huduma za uuguzi
na ukunga wanakumbushwa kuwa na leseni iliyo kwa mujibu wa sheria ya
Uuguzi na Ukunga Namba moja ya mwaka 2010 na kwa wale watakaoshindwa
kuhuisha leseni sheria inasema kwamba hawaruhusiwi kuendelea kutoa
huduma ya Uuguzi na Ukunga.
“Taarifa imeshapelekwa kwa
wahusika na orodha imetayarishwa kwa wale waliohuisha na wale ambao
hawajahuhisha watakuwa wamejifuta wenyewe na hawatokuwa na sifa ya
kuendelea kutoa huduma za afya na waajiri wao watatakiwa kuwachukulia
hatua za kuwafuta kazi kwemye vituo vya umma na vile vya binafsi.
Hata hivyo Bi. Agnes Mtawa
aliwakumbusha Wauguzi kuzingatia maadili kwa kufuata taratibu, kanuni na
sheria kwani kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale kuhusu utoaji wa
huduma kwenye vituo vya afya hivyo kuwakutanisha wauguzi wakuu wa Wilaya
kama viongozi na wasimamizi ni chachu katika kukumbushana taratibu na
jinsi ya kusimamia miongozo na kanuni.
Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya
Rais Tamisemi Kalidushi Charles alisema malalamiko mengi yanaelekezwa
kwa wauguzi kwani sehemu kubwa wanaokaa na wagonjwa kwa muda mrefu na
ndio watu wa kwanza kupokea wagonjwa hivyo wanapaswa kusimamia sheria,
huku akisisitiza kuwa wasioneane haya bali wawajibishane ili huduma za
afya ziwe nzuri.
“Tunafahamu sasa hivi serikali ya
awamu ya tano imeboresha miundombinu kumekuwa na vituo vingi vya kutolea
huduma za afya ambavyo vinafanya upasuaji kwahiyo vituo hivi havitokuwa
na maana kama sisi wasimamizi wa hizo huduma hatutosimamia vizuri ili
wananchi waweze kupata huduma kama adhma yake Rais”.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Wakuu
wa wauguzi ambaye ni Muuguzi kiongozi kutoka Wilaya ya Bukombe Fadhiri
Meshack amesema kuwa, mafunzo hayo yanawajengea uwezo viongozi kwa ajili
ya kupanua wigo wa uelewa ili kuweza kuwasimamia na kuwasaidia wauguzi
wanaowaongoza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...