Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Utafiti cha World Vegetables Center Dr Gabriel Rugalema akitoa Maelezo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina jinsi Viuatilifu vya Asili vinavyoweza kupambana na Visumbufu Shamba wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo Katika Viwanja vya Nyakabindi ,Bariadi Simiyu....Waziri Mpina aliambatana na Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha World Vegetable Center kanda ya Mashariki na kusini mwa Afrika Dr Gabriel Rugelema (Aliyevaa shati la Bluu)Akiteta Jambo na Mtafiti wa Kituo hicho Jeremia Sigalla katika Viwanya vya Nane Nane Nyakabindi ,Simiyu.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha World Vegetable Center aanda ya Mashariki na kusini mwa Afrika Dr .Gabriel Rugelema akimkabidhi Mfuko wa Mbegu Mchanganyiko za Asili Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu wakati wa Maonesho ya Nane Nane.


Na,Vero Ignatus,

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ametembelea Banda la Maonesho la Taasisi ya Kimataifa ya World Vegetable Center lililopo katika Viwanja vya Nyakabindi Vilivyopo Mkoani Simiyu nakujionea Jinsi taasisi hiyo inavyofanya kati katika tafiti ,lishe pamoja na Viuatilifu vya asili na kuonesha kuvutiwa na mbinu hizo.

 Akiwa katika banda hilo Waziri Mpina ameuomba uongozi wa taasisi hiyo kuhakikisha inafikisha mbinu hizo Vijijini nakusema kuwa wananchi wa Vijijini wanahitaji huduma hiyo.

 Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amaesema taasisi hiyo imekuwa na msaada mkubwa kwa wakulima hasa waliojikita katika kilimo cha mboga cha asili hivyo serikali itahakikisha inadumisha ushirikiano.

 Naye Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dr Gabriel Rugalema amesema wao kama wadau wa Kilimo cha Mboga mboga hasa za asili watahakikisha kilimo hicho kinafika Vijijini kama jinsi Waziri Mpina alivyopendekeza.

 Dr Rugalema ameongeza kuwa tayari wameanza mazungumzo na kampuni Tanzu ili kuhakikisha mbinu hizo zinafika Vijijini kwa wakulima ambao watakiendeleza na kuikuza sekta ya Mboga mboga za Asili.

 Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti ya World Vegeteble Center ni Miongoni mwa Taasisi iliyoshiriki Maonesho ya Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...