Na Mwandishi Wetu.

MJASIRIAMALI maarufu nchini, Maida Waziri amebuni mpango wa kuwafanya vijana kufuatilia ndoto zao za ujasiriamali kupitia mradi wa Akili ya Pesa Challenge.

Mradi huo utahusisha uwasilishaji wa mawazo ya ujasiriamali kwa vijana kati ya umri wa miaka 18 hadi 35 na utatumia nguvu ya tehama katika kushirikisha mawazo kiushindani.

“Nia kubwa ya mradi huu ni kuhamasisha ujasiriamali Afrika Mashariki lakini tunaanzia nyumbani. Tunaamini kwamba vijana wana ndoto za kuwa wajasiriamali wakubwa lakini hawana uhakika, sisi tunataka kuwapa uhakika huo ili waweze kuchakarika na kuongeza fursa za ajira,” alisema katika taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari jana.

Mradi huo ambao uko katika mfumo wa Shindano umeanza jana na unatarajia kumalizika Oktoba 15 mwaka huu na mshindi kuondoka kibindoni na Sh 100,000.

Katika mradi huo vijana watakuwa wanaandika mawazo yao ya ujasirimali ya jinsi ya kutumia fursa kukabiliana na mahitaji ya sasa na ya baadaye katika jamii zetu na atakayekuja na wazo zuri zaidi atakuwa mshindi.

Kwa mujibu wa Maida, ili kuwezesha vijana kuwa wajasiriamali ni vyema kubadilisha mitizamo yao juu ya namna ya kuanza na kufuatilia ndoto zao, na Akili ya Pesa Challenge ni muarobaini wake.

“Tunajua, kwa mujibu wa takwimu za NBS kwamba asilimia 60 ya watu nchini ni vijana kati ya miaka 15 hadi 35 hivyo tutatumia nguvu ya Akili ya Pesa Challenge kupanda mbegu ya ujasiriamali ili kuboresha maisha ya vijana, familia na taifa kwa ujumla, na kuifanya Tanzania na Afrika kuwa mahali bora pa kuishi,” alisema.

Akiwa amefanya shughuli za ujasirimali kwa miaka 30, kuhudhuria makongamano 200 ya vijana katika kipindi chote hicho, na kuwahimiza kubadilika na kuwajibika, Maida anajua kiundani zaidi kuhusu matatizo ya vijana na ujasiriamali, tatizo la kujitambua.

“Maneno yangu kwa vijana siku zote ni uanze kidogo na kisha ukue. Haijalishi umeanza na kiasi gani cha mtaji lakini la maana ni kujitambua na kutambua uelekeo wako hivyo kuwa tayari kutekeleza ndoto yako,” alisisitiza Maida.

Anasema Tanzania inakila kitu kinachostahili kuongeza kasi ya uchumi kwa kuwa imebarikiwa na Mungu juu ya raslimali watu na asili .

Anasema kuwapo kwa vitu hivyo kunaweza kabisa , vikitumika vyema, kuingiza Tanzania katika ushindani wa kiuchumi na mataifa yaliyoendele ya Asia.Kwa mujibu wa Maida suluhisho la ukosefu wa ajira barani Afrika (tanzania ikiwamo) ni kuamsha moyo wa ujasiriamali miongoni mwa vijana.

Akili Ya Pesa Challenges imelenga kuweka wazi ndoto za vijana, wajitambue na kuzituamia fursa ili kukabilina na tatizo la uosefu wa ajira.

Akili Ya Pesa kutakuwa na ushindani mwingi na zawadi nyingi za kushinda. Shindano hilo linaanzia katika mitandao ya kijamii kabla ya kupelekwa katika televisheni na radio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...