Na Woinde Shizza ,Michuzi TV Arusha
 
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Karatu imeokoa kiasi cha shilingi million 21 na laki moja za Mwalimu Mstaafu, Fedha hizo zilikuwa zimeporwa na kampuni ya Robby credit Company limited inayomilikiwa na Emmanuel Bonifasi tangu February Mwaka 2019.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda alisema Mzee Pilonga Vicent alienda kukopa fedha kwenye taasisi ya kifedha ya Robby credit kiasi cha million 3 kwa makubaliano ya kurudisha kiasi cha fedha hizo na riba ya 30% ambapo baada ya kuingia kwa fedha yake ya kustaafu million 25 fedha zote zilichukuliwa na taasisi ya Robby credit.

Kayanda alisema vyombo vya habari vimemsaidia kujenga elimu ya uelewa Mzee Pilonga juu ya namna taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa inaweza kumsahidia ,hata ikafanya aweze kwenda kutoa taarifa Takukuru

Aidha alisema Takukuru walichunguza kwa undani jambo la Mzee Pilonga na kugundua kwamba taasisi ya Robby credit ilichukua kadi ya bank na pamoja na numba yake ya siri , hiyo ilichangia fedha za Mzee Pilonga kuchukuliwa na taasisi ya Robby credit.

Kayanda alibainisha watendaji wa Takukuru walilisimamia jambo hilo na viongozi wa Robby credit walikiri makosa waliyoyafanya na kurudisha fedha hizo

Alitoa wito kwa wananchi ambao wamedhulumiwa katika taasisi za kifedha na wanaushahidi wawasilishe malalamiko katika taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ,hata wananchi wanaoenda katika taasisi za umma kupata huduma, kama kuna vitendo vyovyote vinavyoashiria rushwa wasisite kutoa taarifa Takukuru ili kudhibiti vitendo vinavyoharibu taswira ya utendaji kazi.

Awali katika taarifa yake Naibu wa takukuru mkoa wa Arusha Sabasi Salehe alisema matatizo hayo yamezidi kuongezeka mkoani Arusha na wameanza kurejesha fedha nyingi, aliongeza hushughulikia watuhumiwa kwa njia mbili kwanza kwa kuchunguza kwa kina na kujiridhisha kama Mtuhumiwa aliyefanya alifanya pasipokujua, kama ni kweli akirejesha fedha alizochukua anasamehewa na kuonywa.

Alisema kuna watuhumiwa ambao wanavunja sheria ya Takukuru No1 ya mwaka 2017 hivyo sheria inachukuliwa dhidi yao

Kamanda wa Takukuru wilaya ya Karatu Atuganile Stephen alisema wananchi wenye mikopo umiza watoe taarifa ofisini ikiwa ni pamoja na watu wenye taarifa za vitendo vya rushwa kwani jukumu la kupambana na rushwa ni letu sote .

Naye mtaafu aliyerejeshewa fedha zake Mzee Pilonga alisema anajisikia amani yake imerejea kwa sababu alikuwa anawaza analeaje familia kutokana na unyang’anyi haliofanyiwa, lakini kutokana na juhudi za serikali kupitia Takukuru fedha zake zimepatikana, Mzee Pilonga ameishukuru sana serikali kwa msaada aliopata.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Abbas Kayanda (kulia) akimkabidhi Mwalimu mstaafu Mzee Pilonga Vicent juzi million 21 na laki moja ,Fedha zilizookolewa na Takukuru Wilaya ya Karatu Mara baada ya mstaafu huyo kuporwa na kampuni ya Robby credit Company limited inayomilikiwa na Emmanuel Bonifasi tangu February Mwaka 2019 wengine katika Picha Ni maafisa wa Takukuru.(Picha na Woinde Shizza, KARATU).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...