Afisa wa Masoko Bi. Edith James kutoka Plasco Ltd. akielezea umuhimu wa Tuzo za Rais za Mzalishaji bora wa mwaka ( PMAYA) kwa makampuni na kuhamasisha watu kushiriki kama fursa ya kujitangaza na kukuza biashara 
Mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Bwana. Leodegar Tenga akisisitiza ushiriki wa viwanda vidogo na vya kati kushiriki katika mashindano ya Tuzo za Raisi za Mzalishaji Bora (PMAYA).
Afisa wa masoko kutoka kampuni ya ALAF Ltd Bi. Theresia Mmasy akielezea jinsi Tuzo za Raisi (PMAYA) zilivyo za haki na huru

Na Khadija seif, Michuzi TV
SHIRIKISHO la viwanda nchini (CTI) yazindua rasmi shindano la tuzo za Rais za mzalishaji bora wa mwaka wa viwanda kila mwaka maarufu kama "PMAYA" lililopangwa kufanyika novemba mwaka huu.

Aidha, dhumuni la shindano Hilo ni kutambua makampuni kwenye vipengele vya viwanda vikubwa ,vya kati na vidogo.

Akitangaza ramsi kuzinduliwa kwa shindano la PMAYA kwa mwaka huu jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa shirikisho la viwanda nchini (CTI) Leodegar Tenga ,alikaribisha viwanda kushiriki na kuungana na mlezi wa shirikisho la viwanda nchini, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda ifikapo 2025.

"KWA kipindi chote tumepata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau mbalimbali,na kwa mwaka huu tumekwisha pokea idadi kubwa ya washiriki kutoka viwanda mbalimbali kote nchini huku tukihamasisha makampuni mengi ya uzalishaji kushiriki na hususani tunahamasisha ushiriki wa viwanda vya kati na vidogo."

Hata hivyo amesisitiza viwanda kutumia nafasi hiyo kuchangia ukuaji wa biashara zao na kutambulika.

Huku Meneja masoko wa kampuni ya ALAF ltd iliyokuwa mshindi was kiwango kikubwa kwenye kipengele cha chuma na bidhaa za chuma kwenye shindano la mwaka jana ,Theresia Mmasy amesema imekua ikishiriki kwenye PMAYA na kuwa washindi wa vipengele mbalimbali kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.

"Tumeona umuhimu wa PMAYA na ni kwa sababu taratibu zote za ushiriki na mchakato wa kutafuta washindi unafanyika kwa haki na huru Jambo linalotoa nafasi sawa kwa kila mshiriki kushinda."

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya PLASCO ltd waliokua washindi kiwango kikubwa kwenye kipengele cha plastiki na mipira,Meneja masoko na mauzo,Edith James amesema tuzo za PMAYA zimetoa fursa nzuri na ya kipekee kwa viwanda vya ndani.

"Mbali na kutoa fursa nzuri pia imesaidia kukuza ufahamu juu ya umuhimu wa kuhakikisha ubora kwenye sekta zote kwa mtazamo wa kuhamasisha mchango wa viwanda vya ndani kwenye miradi mikubwa ya miundombinu,"

Aidha ametoa rai kwa viwanda nchini kushiriki kwenye shindano hilo kikamilifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...