Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Iringa

WAZIRI Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amempongeza Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli kwa namna ambavyo amefanya kazi kubwa katika kipindi hiki cha kampeni kwa kwenda maeneo mbalimbali kukutana na Watanzania huku akieleza kuwa hana shaka hata kidogo , kwani atashinda tena kwa kishindo.

 Mgombea Urais wa CCM Dk.Magufuli.

Pinda ametoa kauli hiyo leo Septemba 28 mwaka 2020 mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Iringa ambao walijitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni za

"Nakupongeza kwa kazi kubwa ambayo umefanya ya kutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kampeni, sina shaka hata kidogo utashinda tena kwa kishindo.Pia wagombea ubungea na diwani kutoka CCM nao watashinda,'amesema Pinda na kuongeza ukiona vyaeleea ujue vimeundwa.

"Naomba nitumie muda mfupi sana kutoa shukrani kwa ujumla, tumejipanga vizuri na wingi wa watu hawa ni kiashiria tutashinda, tunajua idadi ya wajumbe wa mashina kwa uhakika, mabalozi waliosimama umewaona, tuna kamati kamati ya ushindi kuanzia ngazi ya kati hadi katika jumuiya za Chama,"amesema Pinda.

Pinda ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa, ametumia nafasi hiyo kumueleza Dk.Magufuli kuwa hakuna mahali ambako hajatembelea, amefanya kazi kubwa ya kuondoa tofauti zilizokuwepo na CCM wote ni wamoja na na yoyote anaweza kupeperusha bendera.Pia amempongeza mgombea ubunge wa Iringa Mjini Jesca Msambatavangu kwani ni mwana mama jasiri na ana uhakika atashinda katika nafasi hiyo.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Dk.Magufuli ndio jembe lao , mtumishi wa wote na hivyo Chama kinaomba watanzania wote wamrudishe kwa miaka mingine mitano. "Tumshike sana Magufuli, hapa Iringa Mjini tunayo kazi ya kufanya , Iringa mjini tuna jambo letu, Iringa mjini mnastahili kilichobora , mambo yote ni Jesca Msambatavangu."

Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Dk.Abel Nyamahanga amesema wanafahamu Dk.Magufuli yupo kwenye mikutano ya kampeni ya , atashinda na kwa wananchi wa Iringa wameshamuelewa na watamchagua.

"Iringa wanatoa shukrani sana, katika sekta umeme vijiji 37 tu ndivyo ambavyo havina umeme kati ya vijiji zaidi ya 300, hospitali tatu za Wilaya zimejengwa, zahanati 23 zimejengwa.Chanda chema huvishwa pete, kwa kazi ambayo Rais umefanya unastahili kupewa nishati, jina lako limeng’ara kwa watoto ,wazee hata vijana.Wewe wewe umetuheshimisha wana iringa, umetuheshimisha watanzania, umekuwa mtiifu , tunakupa tena. hatuwezi kukabidhi nchi hii kwa watu ambao wanataka kujifunza,"amesema Dk.Nyamahanga.

Pia amesema Iringa wanajuta na sasa wana tubu kwa kuchagua upinzani, hivyo amesema hawatarudia tena makosa. "Tutakuta kura Rais za kishindo, tutachagua wabunge na madiwani wa CCM ili wawe mikono yako na vidole vyako katika kufanya kazi ya kuleta maeneeleo."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...