Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Tanga Mjini atahakikisha anaboresha soko la Uzunguni lililopo kata ya Central kuwa na hadhi pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za Sekondari Mkwakwani na Old Tanga zilizopo Kata ya Central.


Mgombea Ubunge Ummy akizungumza katika mkutano uliohudhuriwa pia na Mstahiki Meya wa Zamani Alhaj Salim Kassim Kisauji ambae ni mzee maarufu Jijini Tanga amewahikishia wana Central sambamba na kuboresha miundombinu ya shule, barabara za ndani ya kata lakini pia ataangalia uwezekano wa kujenga Zahanati katika kata hiyo ili kuwasogezea huduma za Afya karibu wananchi.


Katika hatua nyingine Ummy amepokea kilio cha watu wa Central kuhusu uchakavu wa nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) ambazo zinakaliwa na wakazi walio wengi wa kata hiyo na kuahidi kuongea na Uongozi wa NHC ili kuzifanyia ukarabati nyumba hizo.

 

 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...