Na Lusajo FrankMaisha ya mshambuliaji wa Arsenal na raia wa Gabon, Pierre Aubameyang huenda yakawa mafupi ndani ya klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika January 2021, na mazungumzo kuwa magumu baina ya pande zote mbili. Kwa mujibu wa gazeti la Uingereza, The Athletics.
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta bado anahitaji huduma ya mchezaji huyo, kuendelea kukipiga klabu hapo kwa misimu mingine zaidi ili kuendelea kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
Aubameyang amekuwa na msimu mzuri ndani ya kikosi cha Arsenal na pia amefanikiwa kuweka kambani magoli 29 na kutoa pasi za magoli 3 katika michezo 44 aliyocheza msimu uliopita 2019/20, pamoja na kombe la FA.
Arsenal inalazimika kutumia nguvu kubwa kumshawishi nyota huyo kuongeza kandarasi mpya ya kuendelea kusalia klabuni hapo kabla ya mkataba wake wa hivi sasa kumalizika January 2021, kuna tetesi nyota huyo kuwaniwa na vilabu vikubwa barani ulaya ikiwemo, Real Madrid nk.
Ikumbukwe Pierre-Emerick Aubameyang alijiunga kwa dau la paundi milioni 56 akitokea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani. January 2018 katika majira ya baridi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...