Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko akikata utepe kuzindua rasmi Maliwato (Changing room) ya kike kwenye viwanja vya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam jana. Benki ya NBCA ilidhamini ukarabati wa Maliwato hayo ya kisasa ili kuwezesha wachezaji Gofu wa kike kupata sehemu nzuri ya kubadilishia mavazi yao. Wengine pichani kulia ni Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwoga, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Resolution Insurance, Maryanne Mugo na Meneja Mkazi nchini wa GardaWorld, Patrick Karimi.
Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwoga akifungua pazia la uzinduzi Maliwato ya kike kwa wachezaji Gofu wa klabu ya Lugalo jijini Dar es Salaaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Maliwato ya kike iliyofanyika klabu ya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwoga (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko (katikati) wakimkabidhi zawadi mchezaji wa Gofu wa klabu hiyo, Chiku Elias aliyejishindia kwa kuwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Chairman Trophy yaliyowashindanisha wachezaji wanawake wa klabu ya Lugalo jana.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko (kulia) akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwoga kwenye hafla ya uzinduzi wa Maliwato ya kike kwenye klabu ya Gofu Lugalo jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...