Cheed na Killy waliozua gumzo mitandaoni siku za nyuma mara baada ya kutoka Kings music kwa kuandika ujumbe unaofanana katika kurasa zao za instagram kwa kudai kuwa wametoka kings music kwa sababu za kifamilia.
Hatimae hatima yao imejulikana hapo jana mara baada ya kujiunga na Konde Gang iliyoko chini ya Konde Boy Harmonize,mpaka sasa konde Gang imefikisha idadi ya wasanii wa nne waliopo chini ya lebo hiyo ambao ni Ibrah, Skales, Killy na Cheed.
Kama kawaida yao Cheed na Killy wameandika ujumbe mrefuu unaofanana katika kurasa zao za instagram kuwataarifu watanzania na mashabiki zao kuwa sasa ni wasanii wa Konde Gang iliyoko chini ya Harmonize.
Kupitia ukurasa wake wa instagram meneja wa Harmonize Mjerumani amewakaribisha kwa kuandika ujumbe ambao ulikuwa unasomeka hivi.
"lengo letu ni kuwapa fursa vijana wenzetu wa kitanzania wenye vipaji ili kwa pamoja kuutangaza mziki wa Tanzania,Afrika na duniani na kumaliza kwa kusema karibuni cheed na killy kwenye familia ya Konde Music World ward".



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...