Mgombea ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi  akiomba kura wananchi wa mtaa wa  Lumwago.
Mgombea ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa kwenye mkutano wa kampeni


Na Fredy Mgunda,Mafinga
MGOMBEA ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi kuendelea kuiomba serikali kuruhusu wananchi kufanya biashara masaa ishirini na manne Kama ilivyo katika kusafirisha mazao ya misitu.

 Akizungumza kwenye mkutano wa wa kuomba kura kwa wananchi wa mtaa wa Lumwago,Chumi alisema kuwa ilikukuza uchumi kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini wanatakiwa kufanya shughuli za kimaendeleo kwa masaa yote ishirini na nne.

Chumi ambaye anayetetea nafasi yake, amesema kama ambavyo Serikali ilikubali kuruhusu malori kusafiri masaa ishirini na manne anaamini Serikali itaridhia wananchi wa Mafinga wafanye biashara masaa 24.

“Huu ni Mji wa kibiashara, sio Saa nne tu polisi hawa hapa wanataka ufunge biashara, haiwezekani, nitaongoza hoja ya kubadilisha sheria Watu wajiachie wafanye biashara usiku na mchana”alisema Chumi

 Alisema Wananchi wa Mafinga wana bidii ya kufanya kazi, kufanya biashara masaa ishirini na manne itaongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, Halmashauri na Taifa kwa ujumla. 

Aidha Chumi alisema wafanyabiashara wanatakiwa kufanyabiashara muda wowote ili kuongeza kipato chao kama ilivyokuwa kwenye nchi zilizondelea hasa kwenye miji midogo inayokuwa kiuchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...