CHUO Kikuu Mzumbe, kimewaalika wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kujisajili chuoni hapo ili waweze kuja kuwa chachu ya kuendelea kukuza uchumi wa kati.

Akizungumza katika maonyeshao ya 15 ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja wa Mnazi mmoja jinini Dar es salaam, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka amesema, kozi zote zinazotolewa na Chuo hicho ni za muhimu sana hasa katika kukuza uchumi wa nchi.

"Unapozungumzia nchi kuingia kwenye uchumi wa kati unakuwa unazungumzia utawala, biashara sheria ujasiliamali na mengineyo ambayo yote tunayofundisha hapa chuoni... hayo ni mahitaji ya zamani na ya sasa kwa sababu hakuna mahali popote duniani unapoweza kuendesha uchumi bila ya kuwa na wataalamu wa fedha na wanasheria, biashara na wajasiriamali.

Amesema Chuo hicho cha Mzumbe kimebobea katika masuala ya utawala, biashara uchumi, ujasiliamali, tehama nk. Na kwamba wahitimu wake wengi wamekuwa wakifanya kazi katika sekta mbali mbali  za umma na binafsi nchini. 

Aidha, Kasulika amewakaribisha watanzania wote vijana ambao wamemaliza shule za Sekondari hivi karibuni, wenye cheti, kuomba kujiunga na Chuo hicho kwani wamejitayarisha kwa ajili ya kuwapokea na kuwapa taaluma itakayowezesha kujiendesha kimaisha.

Ameongeza kuwa Chuo kimekuwa kikifanya maboresho katika matawi yake yote ambapo katika Tawi la Mbeya kunajengwa bweni litakalokuwa na unauwezo wa kuchukua wanafunzi 900.

" Kwenye kampasi kuu maboresho yanaendelea ambapo sasa tunajenga bweni linaloweza kuchukua wanafunzi elfu moja ambalo tunatarajia mwishoni mwa mwaka huu litaanza kutumika kwani serikali iko katika hatua za mwisho kukamilisha na poa Chuo kiko katika hatua ya ujenzi wa madarasa mapya katika matawi yake yote yatakayoweza kuchukua wanafunzi wa ziada elfu moja.

"Tunaboresha sana miundombinu katika Chuo chetu ili kiendane na umaarufu wa jina la Chuo hiki katika maeneo ambayo tunatoa huduma.

Amesema, kuanzia mwaka huu Chuo hicho tawi lililopo Upanga ambalo kwa miaka mingi walikuwa wakitoa shahada ya uzamili (masters) sasa wataanza kutoa shahada ya kwanza.

Pia amesema, Chuo kupitia tawi la Dar es Salaam, wanajenga madarasa mapya eneo la Tegeta ma tunaomba wanafunzi kujitokeza kwa wingi na kujisajili ili waweze kupata elimu ya juu iliyo bora.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe , Profesa Lugano Kusiluka akipata maelezo alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam. Kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Rose Joseph.

 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka akizungumza alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam. Kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Rose Joseph.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka akizungumza na Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.   

 Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe  wakiwadahili wanafunzi katika maonesho ya vyuo Vikuu yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wa kwanza kushoto akiwa na viongozi mbalimbali katika maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu yanayoendele kufanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa akipata maelezo baada ya kutembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 15 ya  vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam(MUSODCC), Aron Msonga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya 15 ya Vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja ya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...