Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
PAZIA la Ligi Kuu Msimu wa 2020/21 Linafunguliwa tena mapema wikiendi hii kwa viwanja vitano nyasi zake kuwaka moto.
Msimu mpya wa Ligi unatarajia kuanza Septemba 06 mwaka huu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezitaka klabu zote za Ligi Kuu msimu huu zenye wachezaji wa kigeni pamoja na watumishi wengine wasio raia wa Tanzania kupeleka vibali vyao vya kazi ili kupata uthibitisho.
Katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu utakaopigwa katika Uwanja wa Majaliwa Mkoani Lindi utawakutanisha Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Namungo dhidi ya Coastal Union, huku Biashara United ikiwakaribisha Gwambina kwenye Uwanja wa
Timu ya Ihefu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu baada ya kuwaondoa Mbao Fc kwenye mchezo wa Play off itawakaribisha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Simba katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, wakati huo huo Dodoma Jiji wakiwa nyumbani dhidi ya Mwadui
Katika mchezo wa mwisho utakaopigwa ndani ya dimba la Mkapa itawakutanisha Yanga dhidi ya Tanzania Prisons.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...