Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Luis Suarez.

Na Agness Francis, Michuzi tv

MSHAMBULIAJI nyota  wa kimataifa Luis Suarez mwenye uraia wa Uruguay ambaye alikuwa akikipiga katika timu ya Barcelona nchini Spain, Ametuhumiwa  na chombo cha uhamiajj  nchini Italia kwa kufanya udanganyifu wa  kuingia  kufanya mtihani wa uraia akiwa na majibu ya mtihani huo.

Kwa mujibu wa sky  Itali imeripoti kuwa  Suarez  alikuwa katika mpango wa kupata uhamisho wa kujiunga na kikosi cha timu ya Juventus nchini humo.

Ambapo mchezaji huyo ilibidi kufanya kwanza mtihani wa kawaida  ili kujua uwezo wake wa kutumia lugha za kiitaliano ili aweze kukizi kigezo cha kupewa pasipoti ya Itali.

Hivyo basi kulingana na uchunguzi wa awali imebainika kuwa maswali yalikuwa katika mtihani tayari Suarez alikuwa amepita mapema, Na hapo ndipo alipotiliwa shaka kwani hawezi kuongea  neno lolote la kiitaliano.

Aidha  upande wa  kikosi cha Juventus  wao tayari wameshakamilisha nafasi za wachezaji wa kigeni ambao hawatoki katika  mataifa ya  umoja wa ulaya kwa msimu huu, Na Suarez  wangeweza kumsajili tu endapo angepata uraia wa Itali

Kwa mujibu wa ripoti ya pande zote mbili zilikuwa zinadai kuwa tayari wamekamilisha makubaliano binafsi, Lakini dili holo limegonga  mwamba kwa sababu ya uraia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...