Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Njombe

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk.John Magufuli amesema amesikitishwa na mauaji ya kikatili yaliyotokea kwa Mwenyekiti wa UVCCM Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa Emmanuel Mlelwa ambapo amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuchunguza tukio hilo na waliohusika wachukuliwe hatua huku akiwaomba

Akizungumza leo mbele ya wananchi wa Mkoa wa Njombe, Dk.Magufuli ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa familia ya Mlelwa, wananchi wa Njombe na wana CCM kutokana na kifo hicho ambacho kimetokea siku za karibuni na kwamba wafiwa wawe na moyo wa subira na uvumlivu.

"Vyombo vya ulinzi na usalama vichunguze tukio hilo ili kubaini ukweli na waliohusika wachukuliwe hatua. Niwaombe wana CCM tufanye kampeni za kistaarabu, tusitukakane mtu, tuendelee kueleza sera na maono ambayo wananchi wa Njombe na Watanzania wanataka kuyasikikia.Katika Uwanja huu kwenye mkutano wapo watu wa vyama vyote na hata wasiokuwa na vyama nao wako, hiyo ndio Tanzania ambayo nataka kuijenga,"amesema Dk.Magufuli.

Amesisitiza katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu ni vema wananchi wakawa watulivu kwa kujiepusha na kila aina ya vurugu huku akifafanua zaidi kuwa Mlelwa kabla ya kufanyiwa ukatili huo alikuwa anakipenda Chama Cha Mapinduzi lakini waliofanya ukatili huo walimua kumchukia kwasababu tu ya mapenzi yake makubwa kwa Chama."Kwa wana CCM hata mkitukanwa msijibu chochote, kikubwa tushikamane, tuwe wamoja  na Oktoba 28 tukawaoneshe kwa kuchagua Rais, wabunge na madiwani kutoka CCM."

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bara Philip Mangulla ametumia nafasi hiyo kuwoamba wananchi na wana CCM kuhakikisha siku ya Oktoba 28 baada ya kupiga kura waondoke nyumbani na wala hakuna sababu ya kulinda kura kama ambavyo baadhi ya wagombea wa vyama vingine wamekuwa wakiwataka watu wao kubaki vituoni kulinda kura.

"Tutakapomaliza kupiga kura siku ile nenda nyumbani, sheria inasema ukipiga kura nenda nyumbani , lakini wenzetu wanahamasishana kuwa baada ya kupiga kura wabaki hapo hapo, hivi kuna mtu anaweza kulinda kura?Kwa utaratibu kuna mtu analinda kura ambaye ni Wakala, na huyo wakala anawakilisha Chama , kura zinamwagwa kwenye meza na kisha zinahesabiwa na kisha mnajaza fomu na baada ya kujaza fomu ya matokeo ndio kila wakala anayotoka nayo, zimebaki siku 29 tu kuelekea siku ya kupiga kura,"amesema Mangulla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...