Miss Tanzania 2000, Mjasiriamali na Muasisi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Ms.Jaqueline Mengi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tamasha la harambee la The Beauty Legacy Tanzania 2020 linalowajumuisha malkia walioshinda Taji la urembo Tanzania lenye lengo la kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia watoto na wamama wenye uhitaji maalumu litakalofanyika Novemba 14 jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala, Miss Tanzania 2001,Happiness Magese, Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari na Miss Tanzania 2018,Queen Elizabeth Makune.
Miss Tanzania 2000, Mjasiriamali na Muasisi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Ms.Jaqueline Mengi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha la harambee la The Beauty Legacy Tanzania 2020. Kulia ni Nancy Sumari na Happiness Magese
Miss Tanzania 2000, Mjasiriamali na Muasisi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Ms.Jaqueline Mengi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tamasha la harambee la The Beauty Legacy Tanzania 2020 linalowajumuisha malkia walioshinda Taji la urembo Tanzania lenye lengo la kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia watoto na wamama wenye uhitaji maalumu litakalofanyika Novemba 14 jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala, Miss Tanzania 2001,Happiness Magese, Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari na Miss Tanzania 2018,Queen Elizabeth Makune.
Miss Tanzania 2018,Queen Elizabeth Makune (kulia) akichangia jambo kwenye mkutano wa wanahabari kuhusu tamasha la harambee la Tanzania Beauty Legacy 2020
Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala (kushoto) akichangia jambo kwenye mkutano wa wanahabari kuhusu tamasha la harambee la Tanzania Beauty Legacy 2020
Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari (wa pili kulia) akichangia jambo kwenye mkutano wa wanahabari kuhusu tamasha la harambee la Tanzania Beauty Legacy 2020.

=========    ==========   ==========


Waliyokuwa Malkia wa Urembo Tanzania wazindua mkakati wa kusaidia afya na elimu nchini Tanzania. 

Tanzania Beauty Legacy 2020, ni mkakati ambao umezinduliwa leo na una lengo la kuwaleta pamoja malikia wa urembo wa Tanzania kuwahamasisha wasichana, wanawake na kuchangisha fedha kusaidia afya na elimu.

Akiongea jijini Dar es salaam, aliyekuwa Miss Tanzania 2000, mjasiriamali na muasisi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Ms. Jaqueline Mengi amesema kuwa alipata hamasa ya kuleta pamoja washindi na washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa nia ya kusaidia jamii.. 

"Tamasha la The Beauty Legacy 2020 litakuwa la aina yake, hafla ya kupendeza ya kutoa sadaka ambayo itawakusanya malkia wa urembo kutoka katika miaka mbalimbali kusherehekea mafanikio yao, kusimulia mapito yetu na kuhamasisha wasichana wadogo nchini Tanzania kuinuka na kutimiza ndoto zao.," Alisema. 


Ms Jacqueline ambaye pia ni msimamizi wa Dr. Reginald Mengi People with Disabilities Foundation amesema kwamba fedha zitakazochangishwa katika hafla hiyo ambayo imepangwa kufanyika tarehe 14 November mwaka huu zitaenda katika kusaidia sekta ya elimu na huduma za afya; ikiwemo kutoa miguu ya bandia kwa watu wanaoishi na ulemavu, vifaa vya kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya umri (watoto njiti) kuishi, kufanya ukarabati wa wodi za wazazi na miradi kama hiyo. 

Aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2001, Happiness Magese alitoa wito kwa wadhamini kutoka katika sekta za umma na binafsi kuunga mkono jitihada hizi za uhisani.

"Wengi wetu tunajihusisha katika shughuli za uhisani na tunaleta manufaa katika maeneo mbalimbali wenyewe. Hata hivyo ninaamini kwamba kufanya kazi kwa kushirikiana katika umoja tutaweza kuleta manufaa makubwa zaidi katika jamii yetu na kuleta maana nzima ya Beauty with a purpose ambayo ni urithi ambao tunataka tuuache katika jamii yetu. Tunampongeza na kumuunga mkono Miss Jacqueline Mengi kwa kutuleta pamoja na kutuonyesha mfumo ambao sote tunaweza kushirikiana pamoja kwaajili ya maono ya pamoja”.

Kwa upande wake, aliyekuwa Miss Tanzania 2005 ambaye ni mwandishi, mfanyabiashara na mjasiriamali wa kijamii, Ms Nancy Sumari alisema kwamba anatarajia kufanya tukio hili liwe ni lenye mafanikio makubwa.

"Kweli hili ni jambo la kihistoria kwa malkia wote wa urembo nchini kwetu kushirikiana pamoja katika jitihada za kusaidia jamii na nchi ambayo ndio iliyotutangaza duniani. Huu ndio msingi wa kweli wa maana ya taji la Miss Tanzania - Urembo wenye Malengo (beauty with a purpose),” alisema.

Tamasha la kuchangisha fedha la BEAUTY LEGACY GALA 2020, usiku wa kusherehekea, urithi na urembo na kurudisha kwa jamii litafanyika tarehe 14 Novemba katika Hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro na linatarajiwa kuvutia watu mbalimbali na wadau kutoka katika taasisi za mashirika, washirika wa maendeleo, serikali na wengine wengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...