Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Prof. Carolyne Nombo wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu huyo alisema TIA wamejipanga vizuri na kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kutoa elimu nchini katika eneo la uhasibu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akipata maelezo kutoka Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Lilian Mpanju Rugaitika wakati alipotembelea maonesho ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Lilian Mpanju Rugaitika akipata akitoa maelezo kwa wanafunzi wa wanaotaka kujiunga na chuo wakati waliotembelea Banda la TIA katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...