Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na
Utafiti wa Madini (GST) Dr Mussa Budeba pamoja na Kamishna Msaidizi wa
Mpango wa Ushirikishwaji wa Wazawa katika sekta ya Madini nchini Terence
Ngole wafanya mazungumzo maalum jinsi ya kuwasaidia wachimbaji wadogo
wa Madini nchini.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika
katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita Dr. Budeba alielezea juu ya umuhimu
wa kuweka kipaumbele katika Mpango wa Ushirikishwaji wa Wazawa katika
sekta ya Madini ili kulinda uchumi wa nchi kwa kutoruhusu makampuni
kutoka nje ya nchi kufanya shughuli zote za uchumi zinazoweza kufanywa
na Wazawa.

Akielezea juu ya Mpango huo Kamishna Msaidizi wa Mpango wa Ushirikishwaji Terence Ngole alisema kuwa ameandaa mkutano na taasisi za fedha na Migodi juu ya kutangaza mahitaji yao na kujua gharama zake kutoka kwa mdhabuni wa nje na ndani ili kupata idadi ya dhabuni zinazoweza kutolewa na makampuni ya wazawa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema kuwa anampango wa kufungua kanzidata juu ya ushirikishwaji wa Wazawa katika sekta ya Madini akishirikisha Taasisi za fedha kwa lengo la kuwasaidia wazawa kwa kuwaboreshea mitaji yao wakiwemo wafanya biashara na wachimbaji wadogo wa Madini.Akizungumzia juu ya wachimbaji wadogo kufanyiwa Utafiti , Mkuu wa Mkoa alisema yupo tayari kutoa eneo la Uwanja kwa GST ili kuweza kujenga Maabara ya Uchenjuaji Madini kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kufanya uchimbaji wa kisasa.
Kikao hiki cha ndani kilijumuhisha pia watendaji wengine kutoka GST na Tume ya Madini.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...