• Ni kuanzia Oktoba 1 hadi 5, 2020
  • Lengo ni kuwapa fursa vijana waliokuwa JKT kuomba
  • …………………………………..
  • Na Mwandishi Wetu,HESLB,

    DAR ES SALAAM

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawajulisha wanafunzi waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hivi karibuni kuwa mfumo wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao utafunguliwa kwa siku tano (05) kuanzia kesho, Alhamisi, Oktoba 1, 2020 ili kuwawezesha kuomba mkopo.


Uamuzi huu unatokana na maombi ya wanafunzi, wazazi na walezi wa wanafunzi wahitaji ambao hawakuweza kuomba au kukamilisha maombi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiunga na mafunzo katika kambi mbalimbali za JKT kwa mujibu wa sheria.


Aidha, katika muda huo wa siku tano, mfumo pia utakuwa wazi ili kuwawezesha waombaji ambao maombi yao yana upungufu kurekebisha kwa kuweka nyaraka sahihi ili kuiwezesha HESLB kuendelea na hatua nyingine.


“Kwa wanaorekebisha taarifa, wanapaswa kuingia katika akaunti zao walizofungua kuombea mkopo na watapata ujumbe kuhusu maeneo ya kurekebisha. Tunawasihi watumie muda huu wa siku tano kurekebisha na kukamilisha maombi yao ili kutuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ili hatimaye wenye sifa wawezeshwe kutimiza ndoto zao,” amesema Mkurugenzai Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru.


Katika mwaka wa masomo 2020/2021, Serikali imetenga TZS Bilioni 464 zitakazowanufaisha jumla ya wanafunzi 145,000. Kati yao, wanafunzi 54,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na wengine 91,000 ni wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo. Mwaka 2019/2020 jumla ya TZS 450 bilioni zilitengwa na zimewanufaisha jumla ya wanafunzi 132,119.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...