Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Simiyu.
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Bariad mkoani Simiyu amesema kwamba Rais Dk.John Magufuli katika kipindi cha miaka mitano ameitendea haki Bariadi, ameitendea haki Simiyu na ameitendea haki Tanzania na kupita kwake kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 28 anatakeleza tu matakwa ya kikatiba.

Chenge amesema hayo leo mbele ya maelfu ya wananchi wa Bariadi na Mkoa wa Simiyu waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Magufli ambaye amefika hapo kuomba kura.

”Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais Dk.John Magufuli nakushukuru sana kwa kuizungumza vizuri ile historia ya mwaka 1995 ya kutoa fedha kwa ajili ya mama Janeth ambaye naye ana upendo mkubwa sana.Sikutegemea kama historia ungeisema vizuri mbele ya watu.”

Amefafanua kwamba mwaka 2005 alipogombea walifanikiwa walifanikiwa kulikomboa jimbo hilo kutoka upinzani.”Tuhakikisha safari hii kura zinakuwa za kutosha sana, nimhakikishie kijana wetu(mgombea ubunge) mimi Andrew Chenge tutafanya kazi ya uhakika.

”Tutambea bega kwa bega kuhakikisha tunapata kura za kutosha, tutakwenda kata zote 31 katika jimbo letu ingawa tayari madiwani wa kata saba wamepita bila kupingwa lakini tutakwenda kutafuta kura kwa ajili yako na wagombea mbunge na madiwani,”amesema Chenge.

Ameongeza ingekuwa sio matakwa ya Katiba Dk.Magufuli unapaswa kuwa Rais wa miaka mingine mitano,kwani ameitendea  haki Bariadi, ameitendea haki Simiyu na ameitendea haki Tanzania.

Kabla ya Chenge kuitwa na Dk.Magufuli ili amuombee kura alielezea historia yake ya miaka mingi inayomhusu yeye na Chenge.”Nawashukuru sana hawa wabunge waliomaliza muda wao, katika siasa kuna miaka 10, lakini nimezungumza maeneo mengi kazi ziko nyingi, Chenge mimi ni kaka yangu kweli kweli wala sio uongo, nilipoingia Bungeni mwaka 1995 mke wangu alikuwa na mimba.

”Aliyenisaidia  hela kwenda hospitali shilingi 200,000 alitoa Chenge, ndio maana nasema sasa nasema ni zamu ya Mhandisi Mfungo, Chenge kazi zipo nyingi,”amesema Dk.Magufuli wakati anamueleza Chenge  na wabunge wengine waliokuwa wakiwatumia wananchi katika majimbo yaliyokuwa katika mkoa huo.
 Mh. Andrew Chenge aliyekuwa mbunge wa Bariadi akimuombea kura na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea Urais Dk.John Magufuli kwa kuizungumza vizuri historia ya mwaka 1995 ya kumpa fedha kwa ajili ya mama Janeth
 Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa

Chama hicho Tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akicheza jukwaani na
vijana wenye ulkemavu wa ngiozi wakati wa Mkutano wake wa hadhara wa
kampeni mjini Bariadi Mkoa wa Simiyu leo Ijumaa Septemba 4, 2020.


 Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni

Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
jukwaa kuu na vijana wenye ulkemavu wa ngozi waliohudhuria Mkutano
wake wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi mkoa wa Simiyu  leo Ijumaa
Septemba 4, 2020

 Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa

Chama hicho Tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya
wananchi katika Mkutano wake wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi mkoa
wa Simiyu  leo Ijumaa Septemba 4, 2020


Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Chama
Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt.

John Pombe Magufuli alipowahutubia katika Mkutano wake wa hadhara wa
kampeni mjini Bariadi mkoa wa Simiyu  leo Ijumaa Septemba 4, 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...