NA VICTOR MASANGU, BAGAM,OYO
Jopo la wataalam wa Afya kutoka Chuo
cha Afya Muhimbili (MUHAS) kupitia program ya ya selimundu wakiongozwa na Dk.
Agnes Jonathan, hatimaye wameanza rasmi zoezi la utoaji wa huduma katika kliniki maalum kwa wagonjwa wa
sikoseli katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani.
Lengo la kuanzishwa kwa utaoji wa
huduma hiyo imekuja ikiwan imepita miezi
miwili tu tangu Serikali kuzindua mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye
ugonjwa wa sikoseli mnamo Juni 19,2020 kwa lengo la kuweza kusaidia kutoa huduma kwa
wagonjwa mbali mbali wanaosumbuliwa na sikoseli katika Wilaya hiyo.
Katika kukabiliana na ugonjwa huo Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
aliagiza kuanzishwa kwa kliniki maalumu
za kuchunguza ugonjwa huo katika ngazi ya wilaya na mikoa ili kuhakikisha watu
wengi hasa watoto wanafikiwa kwa urahisi kupatiwa huduma hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu
Mganga mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mohamed Farah alisema kwamba anashukuru sana
kwa kuzinduliwa kwa mpango huo ambao utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa
wagonjwa ambao wamekuwa wanasumbulia kwa kipindi kirefu na kusumbuliwa kwa sikoseli.
“Kwa
kweli
napenda kutoa shukrani zangu za kipekee kwa kuanzishwa kwa utoaji wa
huduma hii
katika hospitali yetu ya Bagamoyo kwani kutaweza kutoa fursa ya kipekee
kwa
wananchi wa Bgamoyo kupitia wataalamu ambao wamefika kupata huduma ya
matibabu ya sikoseli ambapo wataondoka na changamoto ya kwenda
kutibiwa sehemu
nyingine,”alisema Dk. Farah.
Pia
alifafanua kuwa kuzinduliwa kwa kliniki hiyo katika Hospitali ya Bagamoyo
kupitia mpango ambao umeanzishwa na serikali kutawapa urahi kwa wagonjwa mbali
mbali ambao wanasumbulia na sikoseli kupata matibabau yao kwa uharaka zaidi
kuliko na ilivyokuwa katika kipindi cha
mwanzoni.
Naye
mratibu wa program ya sikoseli kutoka Chuo kikuu cha afya Muhinbili (MUHAS)
Dk.Agnes Jonathan alibainisha kwamba jamii hususan wazazi kuwapelekea watoto
wao mapema kupatiwa matibabu ya sikoseli endapo watabaini kuwa anadalili za
ugonjwa huo lengo ikiwa ni kumpatia matibabu ya haraka.
“Kumekuwepo
kwa baaadhi ya jamii kuwa na mwennendo wa tabia ya kuwa na dhana ptofu
kuhusiana na ugonjwa huu wa sikoseli lakini ni vizuri tukajiwekea utaratibu wa
kuwapeleka wagonjwa hospitalini ili waweze kupatiwa matibabu ikiwemo sambamba
na kwenda kupima afya zao mara kwa mara,”alisema Dk. Agnes.
Bi. Arafa
Said ni Mwanzilishi na Rais wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojulikana kwa
jina la Sickle cell Disease Patiebts Community of Tanzania amewaomba wazazi na
kuwatia moyo wenye watoto ambao wanasumbuliwa na ugonjwa huo waondoe hofu na
mashaka kwani wakizingatia ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya wanawezeza
kusihi maisha marefu bila tatizo.
Mwongozo
wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa Sikoseli ulizinduliwa rasmi Juni
19 mwaka huu na Waziri wa afya maendeleo jinsia wazee na watoto Mh. Ummny
Mwalimu katika hospitali ya Taifa ya muhimbili ukiwa na kauli mbiu inayosema “Huduma
bora kwa kila mhitaji, chukua hatua panua wigo.

Baadhi ya Wataalamu wa huduma za ugonjwa wa sikoseli kutoka chuo cha afya
(MUHAS) wakiwa katika hospitali ya Wilaya ya Bgamoyo kwa ajili ya kutoa huduma
ya matibabu katika kiliniki maalumu ya ugonjwa huo ambayo itakuwa inapatikana
kila siku ya jumatatu.
Dk. Agnes Jonathan ambaye ni mratibu wa huduma ya Sikoseli kutoka Chuo cha afya
Muhimbili (MUHAS) akitoa elimu kwa baadhi ya wagonjwa waliokwenda kupatiwa
matibabu juu ya ugonjwa wa sikoseli sambamba na kuwaelekea namna ya wazazi
kuwahudumia watoto wao pindi wanapokuwa na ugonjwa huo.
Dk. Agnes Jonathan ambaye ni mratibu wa huduma ya Sikoseli kutoka Chuo cha afya
Muhimbili (MUHAS) akifafanua jambo kwa wazazi, walezi pamoja na wananchi
wengine ambao walifika katika kiliniki maalumu ambayo imezinduliwa kwa ajili ya
kutibu ugonjwa wa sikoseli katika hospitali ya Bagamoyo.(PICHA ZOETE NA VICTOR
MASANGU)




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...