Mkuu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Profesa Hozen Mayaya akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ushiriki wa maonesho ya vuo vikuu yanayofanyika katika  viwanja vya mnazi Mmoja.
Msajili wa Wanafunzi Profesa Mwabless Malila akitoa maelezo namna wanavyotoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwa wahadhili wabobevu katika Nyanja ya mipango.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MKUU wa Chuo cha Mipango ya  Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya   amesema kuwa kada ya mipango ni chachu ya maendeleo na hivyo wataalamu wa mipango ya  maendeleo wanahitajika sana hasa katika kipindi hiki ambacho serikali imewekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo. 

Kwa kutambua hilo amesema Chuo kimejipanga kuendelea kutoa mafunzo ya masuala ya mipango kwa wadau wengi kadri iwezekanavyo. "Tupo hapa kwenye maonesho ya TCU ,  Mnazi Moja, Dar es Salaama kwa lengo la kuwasogezea karibu huduma ya udahili kwa  wahitaji wa kozi zetu husuasani wahitimu wa kidato cha sita, diploma na kidato cha nne ili waombe moja kwa moja". 

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho haya,  Profesa   Mayaya amesema kushiriki  katika maonesho haya kunatoa fursa kwa Chuo kukutana na wadau wake kwa ajili ya kuoata mrejesho na pia  kubadilishana uzoefu na taasisi nyingine za elimu ya juu za ndani na nje ya nchi katika nyanja ya utoaji na uendeshaji wa mafunzo katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia.

 Aidha, ameleza kuwa wanatumia maonesho hayo kuifahamisha jamii mchango wa Chuo katika kuleta maendeleo endelevu katika jamii ambapo amebainisha kuwa  Chuo kimendelea kujikita  katika  huduma ya kutoa ushauri elekezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.  Prof . Mayaya amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hususani UNDP watajenga kiwanda cha kugandisha  barafu huko Kanda ya Ziwa katika kuchochea maendeleo ya uvuvi wa samaki kwa jamii ya kanda ya ziwa ilikuwezesha uhifadhi  salama wa samaki kwa ajili ya matumizi ya ndani na kusafirisha nje ya nchi.

Kwa upande wa utafiti Chuo kimeendelea kufanya tafiti mbalimbali kwa lengo la kutatua changamoto za kimaendeleo zinazoikabili jamii ikiwemo sekta ya kilimo.  Moja ya matunda haya ni mradi wa uongezaji wa thamani ya zao la vitunguu swaumu kule Mbulu na ujenzi wa kiwanda cha kukamua alizeti katika wilaya ya Kondoa. 

Katika hatua nyingine Profesa Mayaya  amempongeza Rais Dkt. John  Pombe Magufuli kwa kuifikisha nchi katika Uchumi wa kati kabla ya mwaka 2025 kama ilivyokusudiwa. "Hii inatupa deni kubwa sisi taasisi za elimu ya juu  kuwa tunapasa kuandaa mitaala inayoendana na kazi ya utendaji kazi wa Rais wetu" alisema na kuongeza  "Sisi Chuo cha Mipango tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi wa hali ya juu ili kuisaidia  Serikali ya Awamu ya Tano inafikia adhima yake ya  kuleta mapinduzi ya kichumi kwa watu wote". 

 Profesa Mayaya alisema kuwa  " jukumu letu ni kuwawezesha wanafunzi wetu kufanya mapinduzi ya kifikra". Mkuu huyo wa Chuo ametumia fursa hiyo   kuwasihi  wahitimu wenye sifa kujiunga na Chuo cha Mipango ili kupata stadi stahiki katika  kupanga, kusimamia, kutekeleza na  kutathimini mipango ya maendeleo stadi ambayo ni muhimu sana katika kuupaisha uchumi wetu kwenda juu zaidi.

Wakati huo huo   Profesa Mayaya amesema katika maonesho yajayo watakuja na matokeo ya tafiti kama serikali ilivyoagiza ili kuonyesha uhalisia wa vitu wanavyofanya katka Chuo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...