Mchezaji nyota Wa klabu ya Yanga  Carlos Carlinhos.


Na Agness Francis,Michuzi Tv

KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga Zlatko Kmpotic ameeleza sababu za kutomtumia kiungo wao nyota kutoka Angola Carlos Carlinhos kwenye mchezo Wa kwanza ligi kuu vodacom Tanzania bara dhidi ya Wajela jela Tanzania Prisons kuwa mchezaji huyo bado hayupo fit.

Katika ukurasa wa kijamii wa Yanga umeleza kuwa kocha huyo mpya amewahakikishia wanayanga kuwa wakati wa mchezaji huyo utafika na tapata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.

Aidha kocha huyo raia wa Serbia ameeleza kuridhishwa na uwezo wa nyota huyo hodari, Muhimu anahitaji afikie fitness inayotakiwa.

"Sina shaka na uwezo wake ni mchezaji mzuri ana kipaji cha hali ya juu, Lakini nadhani anahitajika kuimarika zaidi, Hayuko tayari kucheza dakika 90, Alimalizia kwa kusema sio yeye tu wako wengine pia tunawaangalia baada ya muda nafikiri tutakuwa na kikosi imara."amesema kocha Zlatko Kmpotic."

Katika muendelezo wa Ligi kuu Yanga ina kibarua cha kuwavaa Mbeya City Septemba 13, 2020 katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar as Salaam majira ya Saa moja jioni akiwa mwenyeji wa mchezo huo .

Ikumbukwe katika mchezo uliopita Yanga ililazimishwa sare ya kufungana gol i1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na kuvuna alama moja, huku Mbeya city wao wakiambulia kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa vijana Wa Kinondoni KMC FC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...