NA DENIS MLOWE,KIHANSI
LICHA
ya kuwepo kwa sheria na Mafunzo yanayohusu afya na usalama
Kazini,lakini bado inaelezwa kuwa watu wengi hufa na kujeruhiwa kazini
kwa kushindwa kuzingatia elimu wanayoipata Hivyo ni wazi kwamba sheria
pekee haziwezi kuleta usalama kazini waajiriwa wanalo jukumu la
kujilinda na kuwalinda wengine.
Akitoa
Taarifa juu ya hali ya Afya na Usalama kazini,Meneja wa kitengo cha
Afya Usalama Kazini wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mhandisi
Fredy Kayega wakati wa hafla ya Kukabidhi Vikombe kwa washindi wa
Shindano la 10 katika siku ya Afya na Usalama kazini iliyoandaliwa na
Shirika hilo alisema jitihada zinaendelea kufanywa na shirika katika
kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa salama ili waweze kufanya kazi na
kuhudumia wananchi kwa usalama zaidi.
Alisema
kuwa kutokana na hali hiyo shirika la Tanesco liliamua kuanzisha
Mashindano ya Siku ya Afya na Usalama Kazini ili kuhamasisha Vituo na
Mikoa inayozalisha Umeme kuzingatia suala hilo kwa Manufaa ya Taifa na
wafanyakazi kwa ujumla.
Alisema
kuwa Msingi wa Maadhimisho ya Afya na Usalama kazini katika Shirika
letu ni kuinua uelewa na kutekeleza adhma hiyo kwa vitendo ili
kupunguza changamoto ya Ajali zinazotokea katika maeneo ya kazi kwa
kufanya hivyo Shirika litaondokana na Madhara kwa wafanyakazi kwa
shughuli zinazofanywa katika kuwaletea wananchi huduma.
Alisema
Mashindano hayo yamekuwa yakisaidia kupunguza athari zinazojitokeza kwa
wafanyakazi wawapo kazini kwa kuongeza Umakini katika maeneo yao ya
kazi tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kwa Mujibu wa Utafiti Uliofanywa
na Idara ya Afya na Usalama kazini imeonesha kutokuwa na uelewa wa
wafanyakazi ambapo katika kipindi cha mwaka 2016 uelewa ulipanda hadi
asilimi 76%,2017 asilimia 78%, na Mwaka 2018 ni asilimia 79% na 2019
uelewa ulifika asilimia 80% hali inayoashiria itasaidia kupunguza
madhara yanyoweza kujitokeza.
“Pamoja
na jitihada hizi na tathimini hizi zinazofanyika lakini kuna changamoto
kubwa inaambatana nazo ikiwemo ajali zinazowakabili wafanyakazi kwa
mfano mwaka 2017/2018 matukio ya Ajali na ndani ya Shirika zilikuwa
58,na kwa mwaka 2018/2019 ajali zilishuka hadi kufikia Ajali 50 lakini
changamoto ikawa kubwa katika kipindi cha mwaka 2019/2020 ajali kazini
zikapanda hadi kufikia 80 zikisababishwa na Magari kwahiyo changamoto
hizi zinatufanya tuendelee na juhudi kuhakikisha tunakuwa salama”Alisema
Kwa
upande wake, Meneja Mwandamizi Raslimali watu wa Tanesco, Francis
Sanguna akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Umeme Tanzania TANESCO alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Afya na
Usalama kazini Shirika lilitengeneza Sera ya Afya na Usalama kazini
mwaka 2008 lengo ikiwa ni kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa salama wawapo
kazini na nje ya kazi ambapo elimu imekuwa ikitolewa ili kufikia lengo
la Ajali sifuri.
Aidha
amewaonya wale watakaokiuka Misingi ya Afya na Usalama Kazini kuwa
sheria kuwa Shirika la Umeme Tanzania halitamvumilia Mfanyakazi yeyote
atakayehatyarisha Usalama kwanamna yoyote ile kwani kwa kufanya hivyo
kutachangia kuongeza nidhamu kwa wafanyakazi.
“Niwaonye
wafanyakazi wa TANESCO Shirika halitasita kumchukulia hatua yeyote
atakayeshindwa kuzingatia Sheria za Afya na Usalama Kazini na
kusababisha madhara kwa wengine hivyo kila mmoja azingatie kuwa Afya na
Usalama kazini ndiyo msingi wa Maendeleo ya Taifa”alisema
Nao
Levocatus Meshack ni Meneja wa Kituo cha Uzalishaji Umeme cha Kihansi
na Clement Mwakalosi ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Shirika
hilo walieleza namna hatua zinavyochukuliwa kwa kuhakikisha Huduma za
Umeme zinaendelea kutolewa kwa kuzingatia Afya na Usalama kazini na
kuleta Maendeleo Nchini kwani juhudi kubwa ni utoaji wa elimu jambo
lililowafanya kuwa washindi wa Kwanza katika shindano hilo kwa Upanbde
wa Vituo vya Kuzalisha Umeme.
Washindi
katika shindano hilo ambalo ilibidi lifanyike mwaka huu mapema
liliarishwa kutokana na ugonjwa wa Covid 19 kwa Mwaka 2018/2019 kwa
upande wa Vituo vya Kuzalisha Umeme na Kwa Upande wa Mikoa Mkoa wa
Katavi ndiyo ulifanikiwa kushinda ukifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma na
Mshindi wa Tatu ambao ni Mkoa wa Kinondoni Kusini na kituo cha Kidatu
ambao ndiyo waliokabidhiwa vikombe.
Meneja
Raslimali Watu (kushoto) Mhandisi Francis Sangunaa akikabidhi mmoja wa
washindi wa Mikoa Kombe baada ya kufanya vizuri katikaIsimamizi wa
masuala ya Afya na Usalama Kazini
Baadhi
ya Washindi wa Shindano la Afya na Usala Kazini kutoka vituo na Mikoa
mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baadae ya kukabidhiwa Vikombe
Picha
ya Pamoja Baina ya wafanyekazi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO
baada ya Hafla ya kukabidhiwa Vikombe Washindi wa Shindano la Afya na
Usalama Kazini Hafla iliyofanyika katika Kituo cha Kuzalisha Umeme Cha
Kihansi.
Mhandisi
Fredy Kayega Meneja wa Kitengo chá Afya na Usalama Kazini TANESCO
Akizungumza katika Hafla ha Kuwapongeza Washindi wa Mwaka 2018/2019
katika kusimamia masuala ya Afya na Usalama Kazini Hafla iliyosogezwa
Mbele kutokana na Janga la CORONA. (Picha na Denis Mlowe)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...