Na Lusajo Frank, Michuzi TV, Dsj
LIGI kuu nchini uingereza imerejea tena wiki iliyopita, kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbali mbali.
Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta waliibuka na ushindi mnono wa magoli 3-0 dhidi ya Fulham, mchezo uliopigwa katika dimba la Craven Cottage, London.
Mabingwa watetezi Majogoo wa jiji liverpool walipata ushindi wa magoli 4-3 kwa mbinde mbele ya Leeds United mabingwa wa Championship, mchezo uliopigwa katika dimba la Anfield.
West ham United walipokea kipigo cha magoli mawili kwa sifuri kutoka kwa Newcastle united katika uwanja wao wa nyumbani.
Ligi hiyo iliendelea siku ya jumapili, Tottenham Hotspur walipokea kipigo cha goli 1 kwa sifuri kutoka kwa Everton, mchezo uliopigwa katika dimba la White hart.
West Bromwich Albion walipokea kipigo cha goli tatu kwa sifuri kutoka kwa Leicester city katika uwanja wao wa nyumbani.
Ligi hiyo inaendelea tena leo kwa michezo kadhaa kupigwa, Sheffield United watawakalibisha Wolverhampton wanderers, mchezo utakaopigwa majira ya saa 2 usiku na Brighton watawakalibisha Chelsea (The blues) mchezo utakaopigwa majira ya saa 4:15 usiku.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...