MGOMBEA udiwani wa Kata ya Endiamtu, Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara, Lucas Chimbason Zacharia amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kukiangalia kwa jicho la huruma kituo cha afya Mirerani na kukifanya
kuwa hospitali teule kwani kinahudumia wagonjwa wa kata zaidi ya sita.
Luka
akizungumza kwenye ufunguzi wa kampeni ya CCM katika viwanja vya
getini Songambele getini mji mdogo wa Mirerani katika anasema kituo
hicho cha afya kimezidiwa.
Anasema
kituo hicho cha afya kinahudumua wananchi wa mji mdogo wa Mirerani na
kata za Naisinyai, Shambarai, Mbuguni, Makiba na Majengo.
Anasema
dawa zinazofikishwa kwenye kituo hicho cha afya hazikidhi mahitaji
kwani ni kidogo tofauti na idadi kubwa ya watu wanaopatiwa matibabu
pindi wakiugua.
"Mheshimiwa
Waziri Mkuu Majaliwa, pamoja na wananchi wa kata hizo bado wachimbaji
madini ya Tanzanite wanapatiwa huduma za afya katika kituo hicho hivyo
kiongezewe nguvu," anasema Luka.
Anasema
kituo hicho cha afya Mirerani kina eneo la ekari 15 ya kuweka majengo
hivyo kikipatiwa hadhi ya kuwa hospitali teule kinaweza kukidhi haja ya
wananchi wa watakaopatiwa huduma ya matibabu.
"Kutoka
Mirerani hadi Orkesumet kwenye hospitali ya wilaya ya Simanjiro ni
kilomita 122 na kwenda hospitali ya KCMC mjini Moshi au hospitali ya
rufaa ya Mount Meru jijini Arusha ni kilomita 80," anasema Luka.
Amemshukuru
na kumpongeza Rais John Magufuli kwa kukipatia kituo hicho cha afya
gari la kubeba wagonjwa ambalo kwa namna moja au nyingine kinasaidia
wagonjwa wanaopewa rufaa.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu Majaliwa amemuagiza Mkuu wa mkoa huo Joseph
Mkirikiti kufuatilia hilo la hospitali teule na kutia mkazo suala la
dawa hilo kwani serikali ya awamu ya tano imeongeza bajeti ya dawa kwa
hiyo zinapaswa kuwepo.
Amewataka
wananchi wa eneo hilo kumchagua mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,
Magufuli ili aweze kutimiza matarajio yao kwani mambo mengi ametekeleza
katika miaka mitano ya awali.
Mgombea
ubunge wa jimbo la Simanjiro, Christpher Ole Sendeka amewaomba wananchi
wa mji mdogo wa Mirerani kuungana ili kuhakikisha Zacharia anashinda
udiwani.
Anasema baada
ya mgombea udiwani wa CCM kata ya Mirerani Salome Nelson kupita bila
kupingwa ni wakati wa kuungana na kata ya Endiamtu ili kumnadi Luka
naye ashike nafasi hiyo.
"Ndugu
zangu tuachane na siasa tufanye maendeleo sasa kwa kuchagua diwani wa
CCM, mimi mbunge wa CCM na Rais Magufuli ili tuweze kuimba wimbo mmoja,"
anasema Ole Sendeka.
Mgombea udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Endiamtu
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Zacharia akijinaji kwa
wananchi wakati akiomba kura kwenye ufunguzi wa kampeni uliofanywa na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...