Na Mwaandishi Wetu Mtwara
KITUO cha utafiti wa Kilimo nchini TARI) Naliendele kimewata mabwana shamba wakiwemo maafisa ugani kuwatembelea wakulima wa korosho shambani mwao na kuwapa elimu sahihi kuhusu ulimaji na ukuzaji bora wa korosho.

Rai hiyo imetolewa na mtafiti upande wa wadudu na magonjwa kwenye mikorohos kutoka kituoc cha TARI Naliendele Dadili Majune wakati akitoa mafunzo kwa wakulima wa korosho Masasi jinsi ya kudhibiti wadudu na magonjwa yanayoshambulia mikorosho.

Majune amesema mabwana shamba wengi huwa hawatembelei wakulima na kuwapa elimu sahihi kuhusu viwatilifu sahihi na njia sahihi ya kukabiliana ugonjwa na wadudu wanaoshambulia mikorosho.

“Mabwana shamba ndiyo wenye jukumu la kuwatembelea na kuwapa wakulima elimu sahihi na matumizi sahihi ya viwatilifu, lakin wengi wao hawafanyi hivyo,” amesema.

Majune ameongeza kuwa hatua hiyo imekuwa ikiwalazimu wakulima wengi kununua viwatilifu na kutumia visivyo katika kuundoa wadudu na kutibu magonjwa ya mikorosho.

Amesema mabwana shamba na bibi shamba wanatakiwa kuwepo mashambani kila mara na kuwasaidia wakulim njia bora za kuboreshe zao la kilimo.

Kwa upande mwingine Dadili ameiomba serikali kuoogeza maafisa kilimo nchini ili waweze kuwa wengi kusaidia wakulima katika kukuza kilimo

Amesema maafisa kilimo waliopo hawatoshi kusaidia wakulima wote nchini. Kwa upande mwingine, wakulima wa korosho masasi wameomba TARI Naliendele kutoa mafunzo ya kuimarisha kilimo cha korosho kwa mwaka mara tatu ili wakulima waweze kujua na kufuatilia ulimaji na mbinu bora za kilimo cha zao la korosho.

“Tunashauri semina ya namna hii iwe inafanyika kwa mwaka mara tatu, kipindi cha maandalizi ya shamba, kipindi cha upulizaji wa dawa na kipindi cha kuokota korosho,” amesema Maida Rashid, mkulima wa korosho Masasi.

Kwa upande mwingine, mkulima huyo amesema, semina hiyo imewaongoza namna bora ya kutumia viwatilifu katika kukabiliana na wadudu na magonjwa yanayoshambulia mikorosho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...