
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, aliyekua Mwenyekiti wa CHADEMA Singida Kaskazini, Frank Petro, baada ya kuhamia rasmi Chama cha Mapinduzi, katika mkutano wa kampeni, uliyofanyika kwenye viwanja vya Ilongero, mkoani Singida, Septemba 15, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa mkono, aliyekua Mwenyekiti wa CHADEMA Singida Kaskazini, Frank Petro, baada ya kuhamia rasmi Chama cha Mapinduzi, katika mkutano wa kampeni, uliyofanyika kwenye viwanja vya Ilongero, mkoani Singida, Septemba 15, 2020. Kutoka kulia ni mdogo wa Frank, Daniel Petro na Mke wa Frank, Bitrina Ibrahim. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa Kata ya Ilongero, katika mkutano wa kampeni, uliyofanyika kwenye viwanja vya Ilongero, mkoani Singida, Septemba 15, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Wananchi wa Kata ya Ilongero, wakimshangilia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia katika mkutano wa kampeni, uliyofanyika kwenye viwanja vya Ilongero, mkoani Singida, Septemba 15, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
MAJALIWA:
TUJITAFAKARI TUNATAKA KIONGOZI WA AINA GANI
MJUMBE wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Singida watafakari
ni aina gani ya kiongozi wanamtaka aiongoze nchi hii.
Ametoa
wito huo leo (Jumanne, Septemba 15, 2020) wakati akizungumza na wananchi
waliohudhuria mkutano wa kuwanadi wagombea wa CCM uliofanyika kwenye viwanja
vya CCM, kata ya Ilongero, wilayani Singida.
"Uongozi
wa nchi siyo jambo la mchezo, siyo jambo la kujaribiwa wala haliendi kwa upepo
na ushabiki. Ni lazima mkae na kutafakari ni nani anafaa kuongoza nchi
hii," amesema na kuongeza: “Tukae tuangalie tulipo na tunapotaka kwenda.
Tujiulize je, ni nani anaweza kutupeleka huko?”
Amewataka
wakazi hao wajihadhari na wagombea ambao wanatumia majukwaa kuanza kuwatukana
wenzao. "Huu siyo wakati wa kutukanana bali ni wakati wa kuelezea sera na
mambo gani atawafanyia."
Ametumia
fursa hiyo kuwaomba wakazi hao wamchague Dkt. John Pombe Magufuli ili aongoze
tena kwa miaka mitano na aweze kumalizia kazi zilizopangwa na CCM kwenye Ilani
yake.
"Nawaomba
wana-Ilongero, wana-Singida Kaskazini na wana-Singida wote ikifika tarehe 28
Oktoba mchagueni Dkt. Magufuli. Sababu za kumuombea kura ni nyingi hasa
kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwa nchi hii. Wote mmeona na kusikia
yaliyofanyika kwenye maeneo yenu."
"Yeye
ni mzuri wa kutabiri na kuyapangilia na kuyafuatilia. Yeye ni mzuri wa kutambua
kero za wananchi wake na kuzitatua. Amejipambanua sana na kuwasihi wasaidizi
wake wazingatie kuwatumikia Watanzania. Sote tumeona, maendeleo yaliyopatikana
ndani ya miaka mitano hayajapata kutokea," amesema.
Pia
alitumia fursa hiyo kuwaombea kura, mbunge mteule wa jimbo la Singida
Kaskazini, Bw. Ramadhani Ighondo na mgombea udiwani wa kata ya Ilongero, Bw.
Issa Mwiru.
Wakati
huohuo, Mheshimiwa Majaliwa amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa
CHADEMA Wilaya ya Singida, Bw. Frank Petro Akunay ambaye ameamua kuhamia CCM.
Bw.
Akunay amehamia CCM akiambatana na mkewe, Betina Ibrahim pamoja na mdogo wake
Bw. Daniel Petro Akunay.
Akizungumza
katika mkutano huo, Bw. Akunay alisema ameamua kurudi nyumbani kwa sababu
zamani alikuwa CCM lakini alipotea njia.
"Nimeamua
kurudi nyumbani na nitachanja mbuga kuhakikisha CCM inashinda sababu mimi ni
mtu wa field. Hapa Singida Kaskazini tuna vijiji 84, vitongoji 435 na kata 21.
Ninavijua vyote. Nakuhakikishia tutashinda kwa asilimia 98 sababu sijarudi kwa
bahati mbaya," alisisitiza.
"Tuna
uhakika wa kupata ubunge kwani anayegombea hatusumbui kabisa. Kwa madiwani,
tumebakiza kata 19 kwani wawili walishapita bila kupingwa."




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...