Charles James, Michuzi TV
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua kampeni za chama hicho katika Jimbo la Chemba, Dodoma ambapo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura za wingi kwa CCM Oktoba 28 mwaka huu.
Katika mkutano huo Waziri Mkuu Majaliwa amewaombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Chemba, Mohammed Monni pamoja na madiwani wote wa chama hicho ili wakashirikiane katika kuwaletea maendeleo watanzania.
Katika mkutano huo uliofanyika katika eneo la Kelema, Majaliwa amewataka wananchi hao kutohadaika na wagombea wa upinzani ambao hawana hata ilani ya uchaguzi na wasio na uzoefu wa kuongoza.
" Wapinzani wasiwadanganye hawana hata ilani ya uchaguzi, kama bungeni yenyewe huwa wanasusia vikao vya kujadili mambo ya Msingi ya wananchi na Taifa letu tukiwapa Nchi wataweza kuongoza kweli? Niwaombe msiwachague viongozi kwa kuwatazama usoni, chagueni watu wanaoweka maslahi yenu mbele na siyo ya kwao binafsi, watu hao wanapatikana CCM pekee.
Nimefanya ziara kwenye vijiji vyote vya Chemba mlinambia kuhusu Maji, tayari tumeshaiweka kwenye mpango wa kuhakikisha tunamtua Mama kichwani, tumetenga fedha ya kutosha tushagundua tatizo la maji Chemba linasababishwa na nini tutatatua, tumetenga zaidi ya Biluoni 1.5 kwa ajili ya kutafuta vyanzo vya maji," Amesema Majaliwa.
Kuhusu sekta ya Afya, Majaliwa amesema watahakikisha kila kijiji kilichopo Wilaya ya Chemba kinapata Zahanati ili kuondoa changamoto ya kukosa huduma ya Afya kwa wakati.
" Rais Magufuli amefanya mambo makubwa sana hapa Chemba, amejenga vituo vitatu vya afya tayari na sasa mkitupa ridhaa tena atajenga Hospitali ya Wilaya ambayo iko kwenye mpango na itagharimu kiasi cha Sh Bilioni 1.8 na ikikamilika tutaleta Milioni 500 za kujaza vifaa.
Hatutaki wananchi wetu watembee umbali mrefu kwenda Kondoa ama Dodoma mjini kwa sababu hapa hakuna Hospitali ya Wilaya tutaikamilisha na itakua na vifaa vyote," Amesema Majaliwa.
Amewaomba wananchi wa Chemba kumpa ridhaa Dk Magufuli ya kuendelea kuwatumikia ili azidi kuwaletea maendeleo kwenye miundombinu, uchumi na elimu ambapo serikali yake kwa miaka mitano imetoa elimu bila malipo kuanzia shule ya Msingi hadi kidato cha nne.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akimkabidhi ilani ya Uchaguzi y chama hiko mgombea Ubunge wa Jimbo la Chemba, Dodoma, Mohammed Monni katika uzinduzi wa kampeni Jimboni humo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho jimbo la Chemba ambapo zimezinduliwa na Majaliwa.
Mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha Mapinduzi Jimbo la Chemba ambapo mgeni rasmi alikua Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma (CCM), Mariam Ditopile (kulia) akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi mgombea Udiwani wa chama hicho Kata ya Mihuji jijini Dodoma ambapo alizindua kampeni hizo.
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi Kata ya Mihuji ambapo alimnadi mgombea Udiwani, Beatrice Ngerangera na kuwaombea kura Rais Dk John Magufuli na mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ,Anthony Mavunde.
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akimuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na Mgombea Udiwani wa Kata ya Mihuji, Beatrice Ngerangera katika uzinduzi wa kampeni za Udiwani Kata hiyo.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...