Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MCHUNGAJI John Martius Nchambi  wa kanisa la EAGT na wenzake 550 wamewasilisha maombi katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam wakiomba kupatiwa kibali cha kuruhusiwa kumshtaki Msajili wa wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na wenzake kwa kupitisha bodi ya wadhamini ya Kanisa la EAGT kinyume cha taratibu.
 
Mbali ya Msajili Mkuu wa Rita, wengine wanaowaomba kuwashtaki ni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Wachungaji wa kanisa hilo, Joshua Wawa, Christomoo Ngowi, Kenneth Kasunga na Peter Madaha.
 
Maombi hayo namba 48 ya mwaka huu yamefunguliwa na Mchungaji huyo na wenzake wakiomba mahakama hiyo ifute uteuzi wa bodi ya wadhamini ya Kanisa la EAGT kwasababu wakati inateuliwa, kulikuwepo na zuio la msajili wa vyama vya kiraia la Machi 5 mwaka 2018 la kuzuia mikutano yote ya kikatiba ya kanisa hilo na kwamba mpaka sasa zuio hilo halijatenguliwa.
 
Waombaji hao pia wanadai msajili wa RITA ndiye mwenye mamlaka ya kufanya uchunguzi dhidi ya ubadhilifu na matumizi mabaya ya mali za kanisa hilo.
 
Aidha kwa upande wake, wakili wa wapeleka maombi hayo, Robert Rutaihwa amesema katika barua ya Agosti 4 2020 iliyotolewa na RITA, RITA inawatambua Wachungaji Joshua, Ngowi, Kasunga na Madaha kwamba kwa sasa wao ndio wanaounda bodi ya wadhamini ya EAGT.
 
Pia kupitia barua hiyo, Rita imetambua mgogoro uliopo juu ya ubadhilifu na usimamizi mbaya wa mali za kanisa hilo na kueleza kwamba tayari wameshaunda kamati ya uchunguzi, imeshafanya kazi na ipo katika hatu za mwisho kukamilisha taarifa ya uchunguzi huo. 

Kufuatia barua hiyo, baadhi ya wachungaji wakiongozwa na askofu Mkuu wa kanisa hilo wameitisha  mkutano mkuu wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya sita ya kanisa hilo kuchagua viongozi wa kanisa la EAGT wakati kuna barua ya Machi 5 ya mwaka 2018 kutoka kwa msajili wa vyama vya kiraia inayozuia mikutano ya kikatiba, vikao na utekelezaji na kwamba barua hiyo haijawahi kitenguliwa.
 
Anadai, Juni 28 mwaka 2019, wakati kukiwepo na zuio hilo, wachungaji hao walikaa na kuteua bodi ya wadhamini na kisha kupitishwa na RITA kinyume na taratibu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...