Wakwanza kulia ni mgombea Ubunge Jimbo la Arusha mjini Kupitia Chama Cha ADA TADEA , katikati Godbless Lema kutoka CHADEMA Pamoja na Mrisho Gambo kutoka Chama Cha mapinduzi wote wakiwa ni wagombea ubunge katika Jimbo la Arusha mjini.

*************************************

Na Woinde Shizza, Michuzi TV Arusha.


Mgombea ubunge Jimbo la Arusha mjini  kupitia Chama Cha ADA TADEA Zuber Mwinyi ameahidi kuchukuwa Jimbo la Arusha mjini na kuwamwaga wagombea wengine ambao Ni Godbless Lema mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Pamoja na Mgombea ubunge wa  CCM katika Jimbo hilo ambaye ni Mrisho Gambo kwani yeye Ni kiongozi makini aliejipanga kuleta Maendeleo Ndani ya Jimbo hilo.

Aliyasema hayo Jana wakati wa uzinduzi wa kampeni wa Chama hicho ambao ulifanyika katika viwanja vya stendi kubwa ya mabasi ya  mkoani Arusha,ambapo Alisema kuwa yeye ni mgombea tofauti na wengine kwani yeye hagawi fedha kwa wananchi  ili wamchague bali anawaambia wananchi nini atawafanyia pindi wanapomchagua.

Alisema kuwa iwapo wananchi wa Jimbo la Arusha mjini wakimchagua atahakikisha anasimamia rasilimali zote za Jimbo la Arusha mjini ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote .

Aidha Alisema kuwa atahakikisha wafanyabiashara wote wanakuwa marafiki na TRA kwa  kuhakikisha wanakadiriwa Kodi zenye viwango vinavyoendana na biashara zao ,ambapo Alisema kuwa atatengeneza mpango maalum wa kurudisha biashara zote zilizofugwa  na hatakaa kila Mara na wafanyabiashara ili kupata njia rahisi na nzuri za kuendeleza biashara zao.

Kwa upande wa bodaboda Alisema kuwa anampango wa kutengeneza mpango mkakati wa Vijana wa usafirishaji ili waweze kupata mikopo ya bajaji na Toyo kwa Bei nafuu na bila riba .

Aliongeza kuwa atahakikisha wamama wote wajawazito wanapoenda kujifungua hawalipishwi kitu chochote kile pale wanapoingia hospitali Hadi pale wanaporuhusiwa kurudi majumbani mwao.

“Kwakuwa elimu Ni kila kitu nitaweka kitengo maalum Cha kusaidia mikopo ya wanafunzi  iweze kupatikana kwa wakati Ndani ya Jimbo letu na kwakuwa elimu ni bure nitahakikisha kila mtoto anaeanza shule mzazi wake hawalipishwi mchango wowote ule na nitaakikisha madarasa yanajengwa ya kutosha na madawati yanakuwa ya kutosha kulingana na idadi ya wanafunzi”Alisema Zuber.

Aliwataka wananchi kuchagua viongozi watakao badilisha maisha yao na wasichague viongozi kwa kuhamasishwa na vyama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...