NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI



MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini ,Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo, anaanza kufuatilia fedha alizochangisha Rais Dkt. John Magufuli kiasi cha sh. milioni 68,935,000 zilizolenga kuboresha shule ya Msingi ya Soga.

Mwakamo ametoa kauli hiyo akiwa kwenye Mkutano wa Kampeni ya kumuombea kura mgombea wa Urais Dkt. Magufuli, yeye nafasi ya Ubunge na Udiwani katani hapo Shomari Minshehe.

Alisema atasimamia ,kuona kazi hiyo ikifanana na fedha zilizochangishwa.

Anaeleza,Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia Halmashauri Kuu chini ya Mwenyekiti wake Dkt. John Magufuli, limepitisha jina lake awe mgombea Ubunge jimboni hapo, hivyo kabla ya Oktoba 28 anaanza kazi ya kufuatilia fedha alizochangisha Rais alipokuwa Soga.

"Wakati Rais Dkt. John Magufuli alipokuja hapa Soga alipokea kero ya uchakavu wa majengo ya shule, binafsi akachangia milioni 5 kisha akaanzisha harambee iliyokusanya shilingi milioni 68,935,000, naomba mwenyekiti uridhie nianze kufuatilia nione matumizi yake na ubora wa majengo," alisema Mwakamo.

"Huu ndio utakuwa utaratibu wangu, popote pale ambapo viongozi wangu ngazi za juu watakapotoa maagizo, nitakuwa mstari wa mbele kufuatilia nione utekelezaji wake, ," alisema Mwakamo.

Aidha mgombea huyo alibainisha,katika ilani ya chama hicho miaka mitano ijayo imeelezea kuifanyiakazi kwa vitendo migogoro inayohusiana na ardhi, huku akiwatoa hofu wakazi wa Soga kuhusiana na migongano yao ya ardhi.

Nae mgombea Udiwani Kata  Soga Sgomari Minshehe alisema kuwa pindi wakazi hao wakiwachagua wagombea wanaotokana na chama hicho, wataungana kuhakikisha wanasimamia changamoto zinazowakabili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...