Navaya James ni mtafiti kutoka Shirika la Pingos Forum anasema mafunzo au mjadala uliodhaminiwa na OXFAM kwa mradi unaoitwa PG2 kati ya Jamii,Serikali,na uliwafikia wanajamii 25 katika vijiji 2 vya Kitue A na Kitue B
Peter Robert ni Legwanani anasema kuwa ataitumia vyema nafasi yake kuwaelimisha vijana wenzake juu ya kutambua na kufahamu aina mbalimbali za ukatili pamoja na kujua madhara ya ukatili
Maria James anasema kuwa amejifunza mambo mengi yeye kama mwanamke ambayo yatamsaidia ,ambapo haitakiwi mtu kufanyiwa vitendo viovu kama kubakwa,unyanyasaji katika jinsia zote mbili,kwa watoto wapate haki yao ya msingi haswa ya Elimu
Magreth Thomas ni mkazi wa Kitoi A amelishukuru shirika la Pingos Forum kwa mafunzo hayo kisha ameahidi kuitumia elimu hiyo kuielimisha jamii yake juu ya masuala ya ukeketeji kwa watoto wa kike na wanawake pamoja na kumwozesha mtoto wa kike kwa ulazima kabla ya umri anasema yeye alikuwa hafahamu kuwa ni kisheria.
Mshiriki wa mafunzo hayo ndugu Abraham Sakita kutoka kijiji cha Kitwai A yeye anasema kuwa mafunzo aliyoyapata juu ya ukatili wa kijinsia yatamsaidi yeye kuwa mfano bora katika jamii yake kwa kuhakikisha wanawake hawafanyiwi ukatili mfano; mila na desturi mbaya ya kimila kupigwa,kubakwa.
MILA POTOFU ,UMASIKINI NI KICHOCHEO CHA UKATILI WA KIJINSIA KATIKA JAMII
Na.Vero Ignatus,Simanjiro
Amesema kuwa mafunzo hayo yalikusudiwa kufikia watu 25 katika kijiji cha kitwai A na Kiwai B katika wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara, lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na usawa katika masuala ya kijinsia ,kwasababu tatizo ni kubwa hivyo wanawake wa jamii ya wafugaji wa asili pamoja na wawindaji wa asili ,wapo nyuma katika masuala yote ya kijamii,maendeleo, na hata haki kwa mujibu wa sheria za kitamaduni
''Tunaposema zilindwe tunamaanisha kwamba kwamfano watoto wa kike wanalazimishwa kuolewa chini ya umri unaohitajika kisheria ,ukeketaji,wanawake wengi kwa mume mmoja,kwa ujumla tunavyozungumza masuakla ya jinsia tunazungumza masuala yote yaliyokatazwa kwa mujibu wa sheria''Alisema Navaya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...