Na Jane Edward Arusha,Michuzi TV
Kutokana na changamoto kubwa ya maji inayoikabili Wilaya ya Arumeru Mashariki wananchi wa jimbo hilo wametakiwa kutorudia makosa kwa kukichagua chama cha Mapinduzi ili kiweze kumaliza kero ya maji inayoikabili Wilaya hiyo
Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Halmamshauri kuu ya CCM Taifa Anna Agatha Msuya wakati akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki John Palangyo
Amesema kuwa zipo kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo ambapo suala la maji limekuwa ni changamoto kubwa ambapo amemtaka mgombea huyo kutatua changamoto hiyo pindi atakapopewa ridhaa ya kuongoza jimbo la Arumeru Mashariki
Viongozi na wanachama wa chama hicho wanawaomba wanachi wa jimbo hilo kutorudia makosa waliyoyafanya kipindi cha nyuma
Mgombea ubunge wa jimbo hilo Daktari John Palangyo anasema jimbo la Arumeru linakabiliwa na changamoto nyingi na hivyo kuwaomba wananchi kumtuma bungeni ili aweze kufikisha kilio chao cha ukosefu wa maji na barabara
Itakumbukwa kuwa mgombea huyo ameongoza jimbo hilo kwa takribani Mwaka mmoja baada ya Mgombea aliyekuwepo Joshua Nassari kukosa sifa za kuendelea kuwa Mbunge wa jimbo hilo kutokana na kutohudhuria Mikutano ya Bunge kwa kipindi kirefu
Hata hivyo Kata 4 za jimbo la Arumeru Mashariki zinatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa maji wa zaidi ya sh.bl 500 unaotekelezwa na serikali kwa Mkoa wa Arusha.
Anna Agatha Msuya Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki John Pallangyo (Picha na Jane Edward, Arusha)
Wakihutubia Wana Arumeru Mashariki katika kampeni za Ugombea Ubunge CCM(Picha na Jane Edward, Arusha)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...