Na Lusajo Frank, Dsj
MGOMBEA wa kiti cha urais kupitia Chadema Tundu Lissu amekanusha kupokea taarifa ya wito kutoka NEC kufika katika kamati ya maadili.

Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imemtaka mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kufika mbele ya kamati ya maadili ya Taifa kutoa ushahidi kuhusu madai aliyotoa dhidi yake.

Mkurugenzi wa wa Uchaguzi Dkt Charlse Muhera amesema kuwa Tume hiyo imesikitishwa na taarifa za uwongo, uzushi na upotoshaji zilizotolewa na mgombea wa urais wa upinzani Tundu Lissu siku ya Jumamosi.

NEC imesema baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli.

"Kitendo cha baadhi ya wagombea wa Rais hasa mgombea wa Chadema Tundu Lissu kuikashifu Tume kwamba itaiba kura zake ni kitendo cha kuidhalilisha Tume na kutaka kuitisha Tume ili isifanye kazi zake kwa uhuru’.’ alisema Dkt Muhera Charlse.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...