Na Lusajo Frank DSJ 
RAIS wa mpito wa Mali Bah Ndaw amemteua mwanadiplomasia Moctar Ouane kuwa waziri Mkuu mpya katika serikali yake mpya tangu alipoapishwa Septemba 26,2020 ingawa serikali yake ya mpito atahudumu kwa miezi 18 yaani mwaka mmoja na miezi sita.

Rais huyo wa mpito nchini mali alipendekezwa na jeshi na kula kiapo hicho ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja baada ya kujiri mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keita.
Ouane alihudumu kama Waziri wa Mambo ya nje wa Mali kati ya 2004 na 2011 katika nchi hiyo.

Alikuwa mjumbe wa kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa kuanzia 1995 hadi 2002 na baadae kuwa mshahuri masuala ya kidiplomasia wa Muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi, Ecowas.

Uteuzi wake huenda ukachangia Mali kuondolewa vikwazo iliyowekewa na Ecowas kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita.

Kiongozi wa mapinduzi hayo Kanali Assimi Goita alikuwa amemteua Bw.Ndaw – ambaye aliidhinishwa rasmi Ijumaa iliyopita kuwa rais wa mpito.
Moctar Ouane

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...