Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAMLAKA ya Hali ya hewa Nchini (TMA), imeishauri Tume Ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhakikisha inafuatilia na kutumia taarifa za Hali ya hewa katika kipindi hiki cha kampeni pamoja na Siku ya Uchaguzi ya Otoba 28 mwaka huu.
Hayo yamesemaa leo Septemba 7, 2020 na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kijazi wakati wa warsha ya siku moja kwa waandishi wa Habari ya kujadili mwelekeo za mvua za vuli Kwa kipindi cha mwezi Octoba hadi Desemba mwaka huu pamoja na athari zake
Amesema endapo taarifa za hali ya hewa zikifuatiliwa kwa umakini itasaidia upanagaji wa kampeni na hata siku ya Uchaguzi pamoja na zoezi la uhesabu wa kuura kutoathiriwa na hali ya hewa.
"Natambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo wanahabari na vyombo vya habari kwa ujumla mtakuwa na kazi nyingi zinazohusisha kuihabarisha jamii juu ya suala hilo la uchaguzi. Pamoja na jukumu hilo napenda niwakumbushe wanahabari na vyombo vya habari umuhimu wa kuendelea kuzipa umuhimu taarifa za hali ya hewa kwani ni za muhimu katika zoezi zima la uchaguzi." Amesema Dkt. Kijazi
Amesema, wagombea na wananchi wanahitaji kujua jinsi hali ya hewa itakavyokuwa ili kupanga vyema mikutano yao ya kampeni. Hata wakati wa uchaguzi wenyewe kazi ya kusafirisha masanduku ya kura itaweza kufanyika vizuri na kwa ufanisi endapo mipango yake itazingatia taarifa za hali ya hewa.
Pia mamlaka imeweka mkazo katika matumizi ya taarifa za hali ya hewa na ambayo mwaka huu kauli mbiu yake ni 'Tarifa mahususi za hali ya hewa kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda'. Ambapo kauli mbiu hiyo ni ya muhimu hasa ukizingatia uhusiano mkubwa wa hali ya hewa na uzalishaji wa malighafi zinazohitajika katika sekta ya viwanda pamoja na umuhimu wa taarifa hizo katika ujenzi wa viwanda.
Ameongeza kuwa, Mamlaka pia imeboresha na imeanzisha huduma za utoaji taarifa mahsusi kwa kushirikiana na wadau husika, ambapo sasa wadau katika sekta ya utalii na madini wameanza kunufaika.
Wakati huo huo TMA imetoa tuzo kwa wanahabari watatu waliofanya vizuri katika kuhabarisha umma kuandika vizuri habari za mamlaka hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi wa TMA Dokta Buruhan Nyenzi amewapongeza wanahabari waliopata tuzo hizo na wanahabari kwa ujumla kwa kuhabarusha puma juu ya m hali ha hewa na kuwasisitizia kushiriki kuzipa taarifa za hali ya hewa kipaumbele zaidi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi akizungumza kwenye warsha ya siku moja kwa wanahabari kujadili muelekeo wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka 2020 iliyoandaliwa na TMA . Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Agnes Kijazi.
Mkurugenzi Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Hamza Kabelwa (katikati) akizungumza kwenye warsha ya siku moja kwa wanahabari iliyoandaliwa na TMA kujadili muelekeo wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka 2020
Kulia kwake na Afisa habari wa TMA Monica Mutoni na kushoto kwake Samwel Mbuya Meneja wa kituo cha Utabiri cha TMA

Mwanahabari Jerome Risasi, akipokea cheti cha tuzo za kufanya vizuri katika kuandika habari za hali ya hewa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Burhani Nyenzi wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na TMA leo Septemba 7,2020 jijini Dar es Salaal. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi
Baadhi ya wanahabari washindi wa tuzo za habari za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wakiwa katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi pamoja na wajumbe wa bodi ya TMA.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...