NA DENIS MLOWE,IRINGA
MASHINDANO
ya soka kugombea kombe la Ngajilo yaliyokuwa yazinduliwe rasmi Machi 22
na kuahirishwa kutokana na kuunga mkono kauli ya serikali iliyotolewa
na waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa katika kupambana na virusi vya gonjwa
hatari la Corona yanafunguliwa leo September 5 kwenye viwanja vya shule
ya msingi Mlandege.
Akielezea
mashindano hayo , Mratibu wa mashindano hayo, Davis Wapalila alisema
kuwa taratibu zote za kuanza mashindano hayo zilikwishakamilika na timu
shiriki zinatakiwa kufika eneo la tukio kuanzia saa Saba mchana wa Leo
kuweza kufanikisha zoezi la ugawaji wa jezi na vifaa kwa timu shiriki.
Alisema
kuwa baada ya zoezi la kufanya usajili kwa kila timu shiriki kumalizika
kilichobaki na kuanza kwa mashindano hayo ambapo mechi ya ufunguzi
Itakuwa Kati ya wapinzani wa Jadi Kitanzini FC na Mshindo fc
Alisema
kuwa timu ambazo zilitarajia kushiriki mashindano hayo ni 32 lakini
zilizorudisha fomu ni timu 16 ambazo zitagaiwa jezi na mpira kwa ajili
ya mashindano hayo yanayosubiriwa kwa hamu kubwa mkoani hapa.
Alisema
kuwa mashindano hayo yatakuwa na zawadi nono kwa timu bingwa ambapo
Kila timu shiriki itapata jezi seti 1 na mpira mmoja kabla ya mashindano
kwa ajili ya maandalizi.
Alisema
kuwa bingwa wa mashindano hayo mwaka huu ataondoka n ash.Tshs
1,000,000/ na Kombe la Ubingwa , ambapo mshindi wa pili Tshs 500,000/ na
mshindi wa tatu ataondoka na Tshs 300,000/.
Wapalila
alisema kuwa zawadi nyingine ni kwa timu yenye nidhamu ambapo
itajipatia Jezi seti moja, Mchezaji bora wa mashindano, Mwandishi bora
wa Radio kipindi cha michezo, Mwandishi bora gazeti upande wa michezo,
blogs na mwamuzi bora wataoondoka na zawadi ya sh,70,000 huku Mfungaji
bora na Mwamuzi bora msaidizi watajipatia 50,000
Kwa
upande wake mdhamini wa mashindano hayo, Fadhili Ngajilo alisema kuwa
kuanzishwa kwa mashindano hayo ni fursa kubwa kwa vijana wote bila
kutazama vyama vyao kushiriki kutangaza vipaji vyao ili timu
mbali mbali kupata wachezaji kupitia mashindano hayo ambayo
wamewashirikisha viongozi mbali mbali wa timu kubwa za mkoa wa
Iringa kufika kusajili wachezaji .
Mratibu wa mashindano ya Ngajilo Cup 2020 ,Davis Wapalila.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...