Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Iringa

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amewaomba wananchi wa Jimbo la Iringa Mjini kuhakikisha katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu wanamchagua mgombea ubunge wa jimbo hilo Jesca Msambatavangu.

Akizungumza mbele ya wananchi wa Mkoa wa Iringa ambao walijitokeza kwa wingi kwenye mkutano wake wa kampeni, Dk.Magufuli ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Jimbo la Iringa Mjini kuhakikisha wanamchagua Msambatavangu ili awe mbunge wa jimbo hilo.

"Nawaomba wananchi wa Iringa Mjini mtuletee Jesca, tumechunguza hata siku za nyuma alikuwa anaonewa alitakiwa awe mbunge, tena amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, hawezi kushindwa ubunge, naomba mniletee Jesca. Iringa msiniangushe, naomba mwaka huu msiniangushe , Iringa imechelewa sana.

"Maendeleo haya Chama lakini tuna kosa connection, Iringa muda mwingi hamna msemaji, sijui mnanielewa? Maendeleo hayana chama, na mimi nawaomba nileteeni Jesca muone ambayo yatatokea, saa zingine mnakikatisha tamaa, huwezi kupeleka chakula kwa mtoto wa jirani wakati wa kwako ana njaa. niwaambie vipi mnielewe?

"Sijui nimuombe Chifu anisaidie kuwaambia lakini sasa soma kwanza ila waeleze watani zangu Wahehe wabadilike lazima waelewe walikotoka, waliko na wanakokwenda . Bajeti zinapopitishwa wao wanapinga, naomba mbadilike leo.Inawezekana Jesca ana matatizo ya kibinadamu.

"Inawezekana sura yake sio nzuri , naomba naomba mnilete Jesca, naomba Jesca aletwe. Iringa ninaipenda, mnaichelewesha. wangapi watamleta Jesca?"amesema Dk.Magufuli wakati anawaomba wananchi hao wachague mgombea huyo wa ubunge ili ashirikiane naye kuleta maendeleo.

Wakati huo huo Dk.Magufuli amesema Ilani yao ya Uchaguzi Mkuu imegusa kila kitu, haikuacha chochote.Pamoja na mambo mengine Ilani imezungumzia pia makazi bora, kwa msingi huo wanaomba wana Iringa na Watanzania wawachague.

"Ni Uchaguzi Mkuu wa kuamua kupata maendeleo au kutopata maendeleo. Ni uchaguzi wa kuamua kupata viongozi ambao watalinda Muungano wetu , umoja na mshikamano au kuwa na viongozi ambao hawapendi Muungano. Ni Uchaguzi wa kuamua tunataka viongozi wazalendo kwa nchi yao au kupata viongozi ambao hawana uzalendo?

"Ni CCM pekee ndio Chama ambacho kinaweza kuleta usawa, bila kubagua dini , makabila kama ambavyo tumeasisiwa.Hivyo Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi kuchagua Rais wa Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , wabunge na madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi tukalete maendeleo zaidi ya haya ambayo tumefanya kwa kipindi cha miaka mitano,"amesema Dk.Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...