Na Amiri Kilagalila,Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe limewakamata vijana
wawili kwa tuhuma za kuvunja Mahakama ya wilaya ya Njombe na kufanikiwa kuiba
vitu mbali mbali ikiwemo sukari kilo 25,Kopyuta mpakato 3 na Mashine ya Pos
inayotumiwa na mahakama.
Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi
mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema vijana hao ni pamoja ni Masood Mang’ombe
na Hamis Ismael ambao miongoni mwao amehusika
na uvunjaji huku mwingine ni mnunuaji kutoka mkoa wa Ruvuma.
“Kuna watu wameenda wamevunja mahakama ya wilaya ya
Njombe ikaibiwa vitu mbali mbali ikiwemo sukari kilo 25,Pos Mashine inayotumika
na Mahakama na Laptop tatu,na washtakiwa wawili tumewakamata”alisema Kamanda
Issa
“Sasa hivi tunangoja utaratibu ukamilike tuwafikishe
mahakamani ili sheria ili ifuate mkondo wake.Yaani watu walivyokuwa majasiri
hawaogopi hata vyombo vinavyowatendea haki kwenda kuwaibia”aliongeza Kamanda
Issa
Vile vile kamanda Issa amesema wamefanikiwa kukamata
mtandao wa watu wanaohusika wizi wa vifaa mbali mbali kwenye Magari zikiwemo
taa,maturubai,Ekseli na Radio zinazoibiwa wakati magari yakiwa yamepaki mkoani
humo.
“Vifaa hivi vinaibiwa kwenye magari,na leo hii tuna
vifaa ambavyo tumewakamata navyo mtandao wa wezi.Tuna maturubai matano ya
magari makubwa ambayo yanasafiri kutoka mikoa mingine,kuna vifaa vinaitwa Ekseli,halafu
pia kuna Starter mbili za skania na kuna radi za gari ndogo kama kuna watu
wameibiwa waje watambue”aliongeza Kamanda.
Kamanda wa polisi ametoa wito kwa wananchi kwenda
kufanya kazi halali na kuto kujihusisha na mali za wizi ili kuepuka matatizo
yanayoweza kujitokeza.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...