MWENYEKITI wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM, Rais
Dkt. John Pombe Magufuli amewaomba wakazi wa Tarakea wamchague Profesa. Adolf
Mkenda kwa kuwa anauwezo wa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo.
Ameyasema hayo
leo (Jumatatu, Septemba 7, 2020) alipozungumza na wakazi wa Tarakea kupitia
simu aliyompigia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akihutubia mkutano
wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Tarakea, wilaya Rombo, Mkoani
Kilimanjaro.
“Watu wa Tarakea
nawaomba mumchague Profesa Mkenda msifanye makosa tena. Profesa Mkenda alikuwa
Katibu Mkuu wangu na amefanyakazi nzuri na mimi nilimruhusu kwenda kugombea
ubunge katika jimbo la Rombo. Rombo nawaomba mnipigie kura, tunataka tulete
mabadiliko makubwa nchini.”
Kwa upande wao,
wakazi wa Rombo amesema wamefurahishwa sana na heshima kubwa waliyopewa na Rais
Dkt. Magufuli hivyo watahakikisha siku ya kupiga kura itakapofika watamchagua
yeye pamoja na mgombea ubunge Profesa Mkenda na wagombea udiwani wote kwa
tiketi ya CCM.
Mmoja wa wakazi
hao Charles Singano amesema anashukuru sana na kumpongeza Rais Dkt. Magufuli
kwa kazi kubwa anayoifanya kwa Taifa la Tanzania na wananchi wake, ameahidi
kumpigia kura na kwamba atahakikisha anawashawishi wakazi wenzake wajitokeze
kwa wingi na kumpigia kura.
Naye, Mary Mlai
amewaomba akina mama wenzake wamchague Rais Dkt. Magufuli ili waendelee kupata
maendelea mazuri zaidi kwa sababu katika kipindi cha miaka mitano ya awali
ameweza kufanya mambo mengi ikiwemo kutoa elimu bure, kutetea wanyonge wakiwemo
wajane na walemavu.
Awali,
Mheshimiwa Majaliwa alisema kuwa, kwa kutambua umuhimu wa huduma bora za afya
katika wilaya ya Rombo Serikali ilishatenga sh. bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi
wa hospitali ya kisasa ya wilaya ambapo pia imetenga sh. milioni 500 kwa ajili
ya ununuzi wa vifaa katika hospitali hiyo.
Kuhusu tatizo
la upatikanaji wa maji safi na salama, Waziri Mkuu alisema Serikali imejenga
mradi wa maji Njoro II (Tarakea). “Serikali imekamilisha mradi huu kwa shilingi
milioni 200 na unatoa huduma ya maji katika eneo la Tarakea. Malengo ya
Serikali kwa sasa ni kutafuta fedha ili kuupanua mradi huo na kuweza kutoa maji
katika maeneo mengine ya Tarafa nzima ya Tarekea”
Mheshimiwa
Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa wilaya ya Rombo mkoani
Kilimanjaro na Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao wamchague Rais
Dkt John Pombe Magufuli ili aendeleze kazi ya kuwaletea maendeleo katika maeneo
yao ambayo tayari ameshaianza.
Naibu
Waziri na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Aggrey Mwanri akimnadi Mgombea ubunge
wa CCM wa jimbo la Rombo, Profesa Adolf Mkenda katika mkutano wa
kampeni uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa kwenye uwanja wa Soko la Holili wilayani Rombo, Septemba 7,
2020.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...