Na Saidi Mwishehe-Michuzi TV-Kagera

RAIS Dk.John Magufuli ambaye pia kwa sasa anaendelea na kampeni za kuomba ridhaa kwa Watanzania ili apate miaka mitano mingine ya kuwatumikia katika nafasi hiyo, amesisitiza atakapomaliza kipindi cha miaka yake 10 ya uongozi hataongeza tena muda na badala yake atapisha wengine kutoka CCM waendelee.

Dk. Magufuli amebainisha hayo leo Septemba 15,2020, wakati akiwa njiani akielekea mkoani Kagera kuendelea na mikutano ya Kampeni ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.Hivyo ameweka wazi kwa mara nyingine tena kwamba akimaliza miaka yake mitano ijayo hataki kuongeza muda hivyo anaomba apewe miaka mitano mingine ili afikishe miaka 10 ya kuongoza nchi.

Amefafanua kuwa kipindi hicho kikifika yeye atapumzika na kuangalia wenzake wanavyofanya kazi."Palikuwepo na Baba wa Taifa,Mwalimu Julias Nyerere alifanya miaka yake akapumzika, akatutoa kwenye ukoloni ,akaja Mzee Hussein Mwinyi nae akaendelea na ruksa akafanya kazi yake katika miaka kumi angeweza kuendelea lakini alisema imetosha akaja."

Ameongeza hata Hayati Mzee Mkapa naye alimaliza miaka yake kumi akapumzika, akaja Mzee Jakaya Kikwete amefanya kazi yake miaka 10 amepumzika."Na mimi nimekuja nimefanya miaka mitano na sasa naomba tena niongezewe miaka mitano ile iliyobaki nikafanye maajabu kwaajili ya maendeleo ya nchi hii."amesisitiza Dk. Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...