Na Jane Edward Arusha Michuzi TV
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Iddi Kimanta amevitaka vyombo vya habari nchini kuhakikisha wanatumia kalamu zao ipasavyo katika kuzingatia maadili katika kuelekea kipindi cha uchaguzi .
Aliyasema hayo Jana wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa 2020 uliofanyika mkoani hapa na kuwashirikisha wawakilishi wa radio wanachama wa shirika la habari za maendeleo Tanzania (TADIO) zisizopungua radio 34.
Kimanta alisema kuwa,vyombo vya habari vina wajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa vina ripoti taarifa ambazo zina faida kwa jamii kwani endapo kalamu itatumika vibaya inaweza ikaleta madhara makubwa katika jamii.
"Waandishi wa habari mnatakiwa kuhakikisha kuwa habari zenu mnapozitangaza lazima ziwe zimezingatia maadili hasa katika kipindi hiki Cha kuelekea uchaguzi ,mhakikishe mnaandika habari ambazo zinajenga uzalendo wa nchi."alisema Kimanta.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya shirika la habari za maendeleo Tanzania (TADIO)Prosper Kwigize alisema kuwa,lengo la maadhimisho hayo kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili fursa zinazopatikana nchini Tanzania na namna ambavyo jamii inatoa kipaumbele kwa vyombo vya habari katika kupata taarifa mbalimbali.
Kwigize alisema kuwa,mkutanao Mkuu wa 74 wa umoja was. Matafaifa ulitangaza kuwa septemba 28 kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya upatikanaji taarifa kwa wote (IDUAI) ambapo mkutano Mkuu wa UNESCO uliridhia maadhimisho hayo mwaka 2015 .
Aliongeza kuwa,katiba ya shirika la habari za maendeleo Tanzania inabainisha umuhimu wa jamii hasa vijijini kupata taarifa ili kuwapa fursa ya kushiriki katika michakato ya maendeleo ,na hii ni kutokana na ukweli kwamba jamii za vijijini zimekuwa katika uzio wa mawasiliano haswa kukosa fursa za kutoa na kupokea taarifa.
Aidha alitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili tasnia ya habari nchini hasa kwa redio za kijamii zinazotoa huduma vijijini kuwa ni pamoja na Ada kubwa ya malipo ya maombi na leseni na hii inapelekea watu wengi wa kawaida wasio matajiri na asa zisizo na wafadhili wakubwa kushindwa kuanzisha vituo vya redio na hivyo kuinyima jamii haki ya kupata habari.
Kwigize alitaja changamoto nyingine kuwa ni kuwepo kwa malipo makubwa yanayotozwa na TCRA kwa vituo vya redio kila mwaka ambayo kimsingi hayalingani na hali halisi ya kipato pamoja na gharama za uendeshaji wa vituo.
Aidha alizitaka mamlaka za serikali za mitaa kuongeza wigo wa ushirikiano kwa redio na waandishi wa habari katika maeneo yao ili kupanua na kuongeza wigo wa upashanaji habari na kusaidia jamii kupata habari.
Kwa upande wake Mshauri na Mkufunzi wa maswala ya habari kutoka shirika la elimu,sayansi na utamaduni(UNESCO) Rose Mwalimu alisema kuwa,katika kusherehekea siku hiyo wameitumia kuwakumbusha wadau mbalimbali pamoja na vyombo vya habari namna na umuhimu wa upatikanaji wa habari .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Iddy Hassan Kimanta, akifungua Mkutano wa Waandishi wa habari, ambao ni wanachama wa TADIO Mkoani Arusha(Picha na Jane Edward Arusha)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...