Uzinduzi wa Kampeni uliofanyika hapo jana Septemba 13 katika kitongoji cha Mdaula Chalinze uliweza kuongozwa na mgeni rasmi ambae ni Mgombea nafasi ya Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Ridhiwani Kikwete,ambae aliweza kunadi sera zake kwa kuhakikisha jimbo la Chalinze linabaki mikononi mwake kwa kuhitaji wananchi wamachagua yeye ili aweze kuendeleza maendeleo katika Jimbo hilo. 

Mbali na hapo alipanda aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ulanga katika Mkoa wa Morogoro ndugu Goodluck Mlinga na kutema cheche zake za kuhakikisha anaunga mkono juhudi za chama chake cha mapinduzi nchi nzima kinapata ushindi kuanzia Madiwani, Wabunge mpaka  Mh. Dkt John Pombe Magufuli kwa kupata ushindi mkubwa Katika kinyang'anyiro cha kiti cha urais, hali ya kuwa ndugu Mlinga amepoteza nafasi ya kugombania ubunge kwa awamu hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...