Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbas akikata utepe kuashiria kuanza kwa matumizi ya kadi za Kielektroniki zitakazotumika kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa, leo jijini Dar es Salaam.
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi amezindua matumizi ya awali ya kadi za kielektroniki zitakazotumika kuingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kadi hizo zitatumika katika matukio mbalimbali ya kimichezo ndani ya Uwanja huo.
Mfumo huo mpya wa kadi ulianza kutumika katika siku ya Simba (Simba Day) na baadae kilele cha Wiki ya mwananchi.
Kadi hizo zitatumika pia kwa matumizi mengine tofauti na kuingua Uwanjani pale mhusika atakapokuwa ameweka salio kwenye kadi hiyo.
Kwa matumizi ya kadi hiyo, kila kadi moja itatumika kununua tiketi moja na itasajiliwa kwa namba ya mtu mmoja tu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...